Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Kusimikwa kwa mtambo wa kufua hewa ya oksijeni pamoja na 'feeling station', Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana {Ilala}, kumeiwezesha hospitali hiyo kujitosheleza mahitaji yake.

Sambamba na hilo, hospitali hiyo pia imeweza kufunga mifumo moja kwa moja wodini kusafirisha hewa hiyo kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji, badala ya kulazimika kubeba mitungi kuipeleka huko.

Yameelezwa hayo leo na Mhandisi Isaya Kapela wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel alipofika hospitalini hapo kuzungumza na watumishi.

"Mtambo wa kufua hewa ya oksijeni una uwezo wa kuzalisha ujazo wa '50 centimeters cubic per hour', ndani ya hospitali kuna 'feeling station' tangu Desemba 3, 2021 imetuwezesha kupeleka oksijeni moja kwa moja wodini," amesema Mhandisi Kapela.

Amesema wameweza kuzalisha mitungi zaidi ya 140 hadi sasa na wameweza pia kuzisaidia hadi hospitali ya Mwananyamala na Temeke.

Amesema huwa wanajaza na mitungi midogo kwa ajili ya matumizi ya gari za wagonjwa 'ambulance' ili kuweza kuwasafirisha.

"Kule wodini tumesambaza mfumo wa gesi ya oksijeni ambayo unawezesha wagonjwa kupata huduma hiyo moja kwa moja kutoka kwenye mtambo wa kuzalisha, hadi sasa tumenaweza kuhudumia wagonjwa zaidi ya 200 kwa wakati mmoja," amesema.

Amesema kabla ya kusimikwa kwa mtambo huo wa kufua umeme, hospitali ililazimika kwenda kujaza nje ambako iliwagharimu kiasi cha Sh. 40,000 kwa kila mtungi mmoja.

"Kwa kusimikwa mtambo huu maana yake imesaidia kuokoa fedha zilizokuwa zinatumika kupata oksijeni nje ya hospitali," amebainisha.

Naye, Mganga Mfawidhi Amana, Dkt. Bryceson Kiwelu amefafanua zaidi, "Wagonjwa 300 wanaohitaji oksijeni kiwango kama lita tano kwa dakika.

".., na wale wanaohitaji oksijeni kiwango cha lita 15 kwa dakika 200 tuna uwezo kuwahudumia.

"Tuna uwezo wa 'kuzalisha' hewa ya oksijeni na kujaza kwenye mitungi, tuna oksijeni hata kukiwa na changamoto tuna akiba.

"Tunasaidia hospitali zinazotuzunguka, tunakaribisha nyingine za binafsi na za umma tutawajazia kwa gharama nafuu," amesema

Amesema hatua hiyo itaongeza chanzo kingine cha mapato kwa hospitali hiyo.

Naibu Waziri, Dkt. Mollel amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya ili kuhakikisha mwananchi anazipata kokote nchini, inapohitajika.

Msomaji wetu wa MATUKIO NA MAISHA BLOG hivi karibuni  tutakuletea makala itayoeleza kwa undani zaidi kuhusu mitambo hiyo. USIKOSE.

Picha kwa hisani ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement