Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Dar es Salaam

Mashine nyingine kubwa na za kisasa kwa ajili ya kupima kipimo cha haraka cha UVIKO-19 {PCR} wasafiri wanaokwenda nchi za Falme za Kiarabu ikiwemo Dubai, zimefungwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere {JNIA}.

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe  amesema mashine hizo zimefungwa na Serikali kupitia Maabara Kuu ya Taifa ya Jamii iliyo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo, Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Dkt. Sichalwe amefanya ziara maalum ya uwanjani hapo kukagua mwenendo wa huduma za upimaji  wa  UVIKO - 19.

Amesema maabara za Tanzania zina uwezo wa kupima UVIKO-19  na majibu yake yana ubora unaokubalika kikanda na kidunia kwa mujibu wa taarifa ya EAC {Jumuiya ya Afrika Mashariki} na vigezo vya Shirika la Afya Duniani {WHO}.

Ameongeza "Tanzania ni moja kati ya nchi 6 za Afrika Mashariki ambayo maabara zake zimefanyiwa utambuzi  na kukubalika na jumuiya hiyo.

"Katika Taarifa ya tathmini ya Ubora wa Huduma za upimaji wa UVIKO-19 iliyowasilishwa mwezi Novemba na EAC, Maabara ya Taifa imepata asilimia 100 ya vipimo vya ubora," amefafanua.

Amesema maabara nyingine za Kanda zikiwa zimepata asilimia 96 - 98 kiwango ambacho ni cha juu ukilinganisha na kiwango cha asilimia 80 kilichowekwa na WHO.

Ameongeza "Kufuatia tangazo la Falme za Kiarabu kutaka wasafiri wanaotokea Tanzania kwenda Dubai, kupata vipimo vya masaa 48 na kisha kumalizia na kipimo cha masaa sita (6) kabla ya safari.

"Nimefika hapa uwanja wa ndege kujionea hali halisi na hali ni nzuri, mashine za kutosha zipo na timu inaendelea na kazi na pia nimeshuhudia eneo la tenti nje ya uwanja ambapo wateja watakapokuwa wanaanzia kupatiwa huduma. 

"Kikubwa wafike mapema na kwa wakati kulingana na muda wa safari zao," amesema.

Meneja wa huduma za afya mipakani, ambaye pia ni msimamizi mkuu wa huduma za afya JNIA, Remidius  Kakuru, amesema Wizara imeendelea kupima wasafri wanaoingia na wanaotoka nchini na zoezi linaenda vizuri.

"Niwasisitize wasafiri kuwa, huduma  imeanza kutolewa tokea tarehe 16 mwezi huu na tayari tunaendelea na upimaji kwa wasafiri wanaokwenda Dubai.

"Tunawasisitizia wasafiri wajitahidi wafike mapema uwanja wa ndege ikiwezekana masaa saba kabla ya safari zao na gharama hizi za kipimo cha pili ni sawa na ile ya kipimo cha kwanza," amesema Kakuru.

Naye Mwandisi Barton Komba ambaye ni Meneja wa JNIA Terminal 3, ameishukuru Serikali kwa kuwezesha mashine hizo kwa haraka na abiria wote kuweza kupima ndani ya uwanja huo.

"Kwa niaba ya mamlaka ya uwanja wa ndege, tunapongeza juhudi za Serikali kwa kuwezesha kuletwa mashine ndani ya siku tatu na abiria wanapatiwa huduma na sasa ndege ya Emirates itaanza kuondoka kwend huko Dubai na tutarudi kwenye shughuli yetu kama ilivyo awali," amesema Komba.

Katika kuhakikisha ndege hizo za Falme za Kiarabu zinaendelea na safari zake hapa nchini, Meneja wa ndege za Emirates Tanzania uwanja wa ndege wa Terminal 3, Bw. Aboubakar Juma amemhakikishia Mganga mkuu wa Serikali kuwa, Emirates itaendelea na safari zake ambapo kwa sasa wanasubiria kukamilika kwa taratibu ndani ya uwanja huo.

"Tunapenda kuujulisha umma kwamba, kutokana na matakwa mapya ambavyo vilevile yamekuja ghafla kutoka Falme za Kiarabu kwa wasafiri kutoka Tanzania wanaokwenda Dubai, wataitajika kupima mara mbili, ikiwemo PCR covid test masaa sita kabla ya safari.

"Tunapongeza uongozi wa Wizara ya Afya kwa kuchukua hatua thabiti sana na za haraka kuhakikisha ili zoezi linaenda vizuri.

"Hapa nje tumeona tenti kubwa limefungwa na sehemu ya kuchukuliwa vipimo, ambapo tutakapokuwa tayari kutangaza kwamba kusafiri wateja wote wanaokwenda Dubai watahitajika kufika uwanja wa ndege masaa saba kabla ya safari wakiwa na  'covid test' zao za kawaida zisizo chini ya masaa 48 na wakifika hapa watapitia eneo hili wakiwa wameshalipa 'USD 50' kupitia malipo ya mtandaoni ilikupunguza usumbufu hapa

Aidha, amesema baada ya taratibu, watatumiwa majibu yao kupitia simu zao kwa kupitia mtandao wa WhatsApp ama email kisha taratibu zingine na safari.

"Wasafiri wanatakiwa kufanya miahadi ya safari zao 'booking'  kupitia mtandaoni katika;

https://pimacovid.moh.go.tz/#/booking na kufanya malipo na kisha kuchagua kituo cha kupima na kupata cheti ambacho kinakuwa tayari ndani ya masaa 48.

Kaimu Mkurugenzi wa maabara kuu ya taifa,  amewaomba wasafiri ambao wanatakiwa kupima uwanja wa ndege ni wale tu wanaokwenda ama kupitia Dubai pekee na wale wengine watatumia utaratibu wao wa kawaida.

"Tulipata mahitaji hayo ya Emites na tukafunga vifaa hapa uwanjani na hadi sasa tayari tumepima abiria Sabina na moja.

Abiria wakifika mapema zaidi itasaidia wao kuwahi safari zao na pia wanatakiwa walipie mtandaoni ilikuepuka usumbufu. 

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement