Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Mwanaume mmoja aliyekuwa akikabiliwa na tatizo la kuziba mshipa wa damu kwenye moyo, amezibuliwa leo kupitia mfumo wa satellite/ mfumo wa mawasiliano kidigitali yaani {tiba mtandao/telemedicine} ndani ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete {JKCI}.

Jopo la wataalamu mabingwa wa JKCI, wakiongozwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Magonjwa ya Moyo, Peter Kisenge, limefanikisha upasuaji huo wa kihistoria kwa ushirikiano na mabingwa wenzao wa Marekani {Madaktari Afrika}.

Upasuaji huo uliotumia saa moja pekee hadi kukamilika, ukiwa live hewani kupitia mtandao wa zoom, haujawahi kufanyika Afrika Mashariki na Kati.

Dk. Kisenge amesema ni hatua kubwa mno kwa Tanzania huku akiishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kuendeleza juhudi za kuimarisha taasisi hiyo.

Katika mahojiano maalum na MATUKIO NA MAISHA BLOG, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi amesema upasuaji huo ulipangwa kufanyika kwa njia hiyo Kutokana na athari za janga la CORONA.

"Wenzetu {madaktari Africa} tumekuwa na ushirikiano nao mzuri wa muda mrefu, hapa JKCI huu ni mwaka wa sita sasa tangu tumeanza huduma kama Taasisi.

"Upasuaji kwa njia ya satellite haujawahi kufanyika nchini mwetu, ndiyo mara ya kwanza," amesema.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement