Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Wataalamu wanaotoa huduma Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala {RRH} wameagizwa kuwapa ushirikiano wa karibu ndugu wa wagonjwa hatua kwa hatua wanapowahudumia ili kuepusha malalamiko kujitokeza.

Wamehimizwa kuimarisha huduma kwa wateja {customer care service} pasipo kukiuka miiko na maadili ya kitaaluma.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Godwin Mollel ametoa maagizo hayo alipofanya ziara ya kawaida ya kikazi hospitalini hapo jana na kuzungumza na wafanyakazi.

Ziara hiyo ya kikazi ya Dkt. Mollel imekuja wakati ambao pia kumekuwako malalamiko kutoka kwa wananchi yaliyosambazwa mitandaoni wakidai kutopewa ushirikiano na wataalamu wa hospitali hiyo.

"Lakini ukichungulia kwa undani kabisa vitu mlivyoandikwa inawezekana mlikuwa sahihi au vifo vilivyotokea mlikuwa hamna uwezo wa kuvizuia.

"Lakini hamkutoa ushirikiano kwa ndugu wa wagonjwa, yaani mtu anapeleka watu kama ma-roboti roboti, ulifika kwa sababu wewe ni daktari unawaambia tokeni, tokeni, hapana.

"Ndugu wa mgonjwa unamfuata, unamuambia ndugu yako ni mgonjwa, ana shida hii, tumeamua kufanya hivi, tumeamua kumlaza hapa au sehemu nyingine, tumeamua kumuweka huku kwa sababu moja, mbili, tatu si ndugu wa mgonjwa ana anaelewa," amesema.

Ameongeza "Wakati mwingine unamuita hata ndugu mmoja unamuambia yupo salama, tunaendelea kupambana kumuokoa mgonjwa.

"Lakini mkianza kuwafukuza mpaka walinzi wanazuia getini, mwisho wa siku likitokea tatizo lolote kwa sababu hujashirikisha ndugu tangu mwanzo, matokeo yake ni haya {malalamiko}," amesisitiza.

Dkt. Mollel ameongeza "Imarisheni huduma kwa wateja {customer care service} pasipo kukiuka miiko na maadili ya kitaaluma.

"Najua kuna 'privacy' {haki ya usiri kwa mgonjwa} lakini shirikisheni vizuri ndugu wa mgonjwa kwa kuzingatia taaluma, utaalamu na miiko ya kazi.

"Washirikisheni ndugu wa mgonjwa yale yanayoweza kushirikishwa ili likitokea la kutokea muwe mpo pamoja.

Awali Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Zavery Benele amesema licha ya kuwa na changamoto karibu huduma nyingi zimeboreshwa na wanafanya vizuri.

"Kwa sasa hospitali tunatoa na kuendelea kutoa huduma za kibingwa ikiwemo idara ya upasuaji, pua na koo, magonjwa ya ndani, magonjwa ya ngozi, kinywa na meno kwa watoto," amesema.

Dkt. Benele amesema hivi sasa kwa siku wanahudumia wastani wa wagonjwa 1600 hadi 2000.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement