Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Veronica Mrema 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Tanzania imethibitisha kuna ongezeko la wananchi wanaopata dalili za mafua, hata hivyo imewatoa wasiwasi , hiyo huwa ni hali ya kawaida kila mwaka (seasonal influenza).

Ingawa takwimu hazijabainishwa wazi kuhusu, imesisitiza hali hiyo huchangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa kama ambavyo iliweza kushuhudiwa kwa miaka mingine iliyopita.

Yameelezwa hayo na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Aifello Sichwale amesema hayo leo ndani ya taarifa yake kwa umma aliyoitoa leo, hilo ni kutokana na uwepo wa taarifa zilizoenea mitandaoni kwamba kuna watu wengi wana dalili za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka.

Amesisitiza katika kuhakikisha umma unaendelea kupata taarifa za mwenendo wa Mafua katika kipindi hiki, Wizara imeshaelekeza taasisi za utafiti za kitaifa kama NIMR, vyuo vikuu na watalaamu wetu kuendelea kutoa takwimu na elimu kutokana na ufatiliaji wa Kisayansi (Survellience) ambao wamekuwa wakifanya kuhusiana na visa vya mafua nchini.

"Wizara na taasisi zake tunaendelea kufuatilia kwa karibu viashiria vya mwenendo wa hali hii. 

"Aidha, Wizara inashauri kuwa wananchi wenye dalili hizi za kukohoa, mafua, maumivu ya mwili na kuchoka watoe taarifa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili wafanyiwe uchunguzi wa kitaalamu na wapatiwe matibabu stahiki," amesema.

Ameongeza "Pamoja na hali hii ya mwenendo wa mafua ya kawaida, vilevile Wizara inaendelea kukumbusha na kutoa tahadhari kwa kila mtu kuendelea kuchukua hatua zote muhimu za kujikinga na janga la UVIKO-19 ikiwa ni pamoja kuepuka misongamano isiyokuwa ya lazima, kunawa mikono, kuvaa barakoa na kuhakikisha kuwa kila mtu anapata dozi kamili ya chanjo. 

"Wito kwa wananchi kutoa taarifa za tetesi za viashiria vya magonjwa ya mlipuko kutoka katika jamii kupitia namba ya simu 199 bila malipo yoyote. 

".., napenda kuwakumbusha kuwa ugonjwa wa UVIKO 19 bado upo na huenda maambukizi ya ugonjwa huu yakaongezeka hasa tunapoelekea mwisho wa mwaka unaohusisha kipindi cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka hivyo.

".., vema tuzingatie kuchukua tahadhari zote kama zinavyoelimishwa na wataalamu wa afya bila kusahau kuchanja. 

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement