Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Maalum

Watu wanaokwenda kusherehekea msimu wa sikukuu ya krismasi na mwaka mpya vijijini wamehimizwa kuhakikisha wanajikinga na kuwakinga/wanawalinda wazee dhidi ya maambukizi ya UVIKO - 19/COVID - 19

Rai hiyo imetolewa mapema leo na Karibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Mpango Shirikishi na Harakishi Awamu ya Pili wa Mapambano dhidi ya UVIKO-19 unaotarajiwa kuzinduliwa Desemba 22, mwaka huu, Arusha.

 “Pamoja na kuongezeka kwa Mafua ya Kawaida (Seasonal Influenza), bado tuna visa vya UVIKO-19 na vinaongezeka kwa kasi," amesema hata hivyo hakijabainishwa wazi takwimu zilivyo. 

Ameongeza "Nawaomba wananchi waendelee kuchukua hatua za kinga zote ikiwemo kuepuka misongamano, kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, kuvaa barakoa na kupata chanjo hasa kuelekea krismasi na mwaka mpya.

"Familia  zinazosafiri kwa ajili ya sikukuu za mwisho mwaka hakikisheni mnawalinda wazee huko vijijini kwa kuchukua tahadhari zote pamoja na kuvaa barakoa na kuchanja," amesisitiza.

Ametoa rai pia kwaa wamiliki wa byombo vya usafiri na vikosi vya polisi barabarani(Trafiki) kuelimisha na kusimamia wananchi kuepuka kujazana katika mabasi na daladala, kuvaa barakoa na kunawa mikono.

"Katika kipindi hiki cha likizo, wazazi tuwaepushe watoto kwenda kwenye sehemu zenye mikusanyiko isiyo ya lazima ili tuwalinde watoto wetu," amehimiza.

Kuhusu uzinduzi wa Mpango huo wa pili, Prof. Makubi {pichani chini} amesema itakuwa kampeni Shirikishia, mtaa kwa mtaa na nyumba kwa nyumba.

Amesema tayari watoa huduma ngazi ya jamii zaidi 8,130 wamepatiwa mafunzo ya namna bora ya kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa chanjo katika kukabiliana na Uviko-19 ili waweze kuchukua hatua ya kuchanja kwa hiyari.

Amesema tayari wameshazielekeza timu za afya za mikoa na halmashauri, kuendelea kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii, viongozi wa dini kimila sambamba pamoja na makundi yote yenye ushawishi ndani ya jamii. 

Prof. Makubi amesema ajenda hiyo ya Kampeni Shirikishi na harakishi ina sura ya kitaifa kwa  Wizara zote za kisekta, aidha kwa kutambua hilo, tayari Ofisi ya Rais-TAMISEMI, imeandaa Mwongozo wa Wawezeshaji na Wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii.

".., ikiwa ni pamoja na kuwatambua wahudumu waliopo katika ngazi ya vijiji, mitaa na vitongoji na kuanza kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo kuhusu afua za kinga dhidi ya UVIKO - 19 na umuhimu wa wananchi kuchanja.

Prof. Makubi ameongeza "Kwa kuwa vita hivi ni vya kila mtanzania basi hata kundi la wanahabari, halina budi kuwa mstari wa mbele kuhamasisha ili kuwezesha kufanikisha kampeni hiyo itakayozinduliwa mkoani Arusha.

Tanzania ilianza kutoa chanjo za UVIKO-19 mapema mwezi Agosti, 2021, chanjo ya Jenssen ikiwa ndio ya awali kabisa kutolewa ikifuatiwa na Sinopharm na Pfizer zenye dozi mbili kwa kila chanjo.

Aidha hadi kufikia Desemba 18, 2021 jumla ya wananchi wapatao 1,275,795 walikuwa, wamejitokeza na kupata chanjo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement