Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Mwandishi Maalum - Mbeya

Kituo cha redio ya mtandaoni Boresha Radio kimeibuka kinara kwenye tuzo za Mamlaka ya Dawa, Vifaa tiba na Vitendanishi (TMDA). 

TMDA imetoa tuzo hizo kwa mara ya kwanza kutambua mchango wa wanahabari katika kuelimisha jamii kuhusu bidhaa hizo ambazo wanazisimamia pamoja na udhibiti wa tumbaku na bidhaa zake.

Boresha Radio imeibuka kidedea kupitia aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Matukio na Maisha, Veronica Mrema, kipindi hicho kilikuwa kinarushwa kila jumamosi na marudio yake jumapili.

Akizungumza, Veronica ameishukuru Mamlaka hiyo kwa kuanzisha tuzo hizo kwani zitachochea kuongeza hamasa kwa wanahabari kuelimisha jamii.

"TMDA ina jukumu la kulinda afya ya jamii na wanahabari pia tunawajibika kwa jamii yetu kuhakikisha tunawapa elimu kuhusu bidhaa hizi.

"TMDA ina wajibika  kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya dawa, kunakuwa na ubora wa vifaa tiba na vitendanishi nchini pamoja na kudhibiti matumizi ya tumbaku na bidhaa za tumbaku.

"Wanahabari tukitumia vema majukwaa yetu kwa pamoja tunaisaidia jamii yetu," amesema Veronica.

Awali akizungumza, Mkurugenzi Mtendaji wa TMDA, Adam Fimbo amewataja washindi wengine ni Mwakilishi wa Mtandao wa Matukio Daima (Blog), Andrew Chale, Waziri Suka wa Tumaini TV, Averine Kitomari Habari Leo na  Grace Mwakalinga mwakilishi wa IPP Media ameshinda tuzo ya jumla.

"Taratibu za kutoa tuzo kwa wanahabari wanaofanya vizuri katika kuandika habari za TMDA, watakuwa wanapewa tuzo hizo kila mwaka kutoka kwetu," amesema.

Awali kabla ya tuzo hizo, kilitanguliwa kwa kikao kazi kwa Wahariri na Waandishi wa Habari, kutoka mikoa ya Njombe, Mbeya, Rukwa na Songwe na Dar es Salaam.

Akifungua kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa rai kwa wanahabari kuendelea kutumia taaluma yao kuelimisha jamii kwa kuipa taarifa zenye tija zitakazojenga Taifa lenye afya.

2 Maoni

Chapisha Maoni

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement