Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Dar es Salaam 

Dawa za kulevya za mashauri ya kipindi cha mwaka 2009 hadi 2022 zimeteketezwa kwa moto baada ya kesi za mashauri hayo kumalizia katika mahakama mbalimbali, Dar es Salaam.

Uteketezaji huo umefanyika leo Desemba 21, 2022 chini ya usimamizi madhubuti wa maafisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya {DCEA} na mashahidi kutoka taasisi nyinginezo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Kamishna Jenerali, Veronica Matikila, amesema jumla ya kilo 2,584.55 za dawa za kulevya.  

Amesema dawa za kulevya zinazojumuisha kilo 569.25 za heroin, kilo 15.3 za cocaine na tani mbili za bangi na mirungi. 

Amesema mashauri hayo yalikuwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, na Mahakama za Hakimu Mkazi za Kisutu na Kibaha Pwani pamoja na Mahakama za Wilaya ya Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni. 
"Dawa za kulevya zilizoteketezwa leo zimehusisha mashauri ya kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2022," amesisitiza.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement