Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Veronica Mrema 

Kijana Maxmillian Godwin aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Desemba 5, mwaka huu alikuwa miongoni mwa vijana walioyaishi waziwazi maono marehemu Dkt. Mwelecele Ntuli Malecela.

Dkt. Mwelecele kabla ya kufikwa na umauti alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele {NTD's}.

Aidha, kabla ya hapo alikuwa ndiye mwanamke pekee wa kwanza kuwahi kuiongoza Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania {NIMR}.

Dkt. Secelela Malecela ambaye ni mdogo wake na  Dkt. Mwelecele ameieleza MATUKIO NA MAISHA BLOG kwamba marehemu Maxmillian alikuwa kijana mwerevu na aliyempenda mno dada yake.

"Alinitumia video akiwa jukwaani baada ya kutunukiwa tuzo {akiwa mshindi wa tuzo za vijana chipukizi Tanzania, mhamasishaji bora wa mwaka katika sekta ya afya Agosti, 2022}," amesema.

Katika video hiyo, Maxmillian anaonekana akisema kwa tuzo hiyo anashukuru na kutambua mchango wa Dkt. Mwelecele kwa vijana kwani alikuwa chachu {role model} kwa wengi juu ya eneo hilo la NTD's}.

Dkt. Secelela ameongeza "Sijawahi kumfahamu Max. sijawahi kuonana naye ana kwa ana, lakini hata wiki chache zilizopita aliwasiliana na mimi.

"Aliniambia hakuwahi mazishi {Mvumi, Dodoma kwani alikuwa safarini}, lakini hivi karibuni aliporudi {Tanzania} aliweza kwenda kuhani.

"Alikuwa kijana mwema kwa namna hii... Kazi ya Mungu haina makosa, kwa hiyo hata katika hili tumshukuru Mungu kwa maisha ya Max.," amesema.

Pamoja na Dkt. Secelela, wadau wengine mbalimbali wameendelea kutuma salamu zao za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Maxmillian.

Uongozi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya African Youth Transformation {AYT} ambayo ndiyo waratibu wakuu wa tuzo za vijana chipukizi Tanzania {TEYA}, katika kurasa zake za mitandao ya kijamii imeeleza kusikitishwa na msiba huo.

"Uongozi mzima wa AYT umepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa kijana Maxmillian alikuwa ni mmoja wa mshindi wa tuzo za TEYA 2022.

"Tunatoa pole kwa familia nzima pamoja na vijana wote kwa msiba huu mzito, 'may his soul R.I.P {Rest In Peace}," wameandika.

Kifo chake kimegusa watu wengi akiwamo Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus, ambaye naye juzi alituma salamu za rambirambi kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya ambako marehemu alikuwa akifanya kazi kwa kujitolea, alisema kijana huyo alikuwa akisoma taaluma ya Ufamasia huko Chuo Kikuu cha Zambia.

DC. Kyobya alisema Maxmillian alipata ajali Desemba 5, mwaka huu akitokea Njombe kuelekea Songea.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement