Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Dar es Salaam 

Wadau wa habari nchini wanafurahia Uhuru wa habari lakini bado haulindwi kisheria.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania {TEF}, Deodatus Balile amsema hayo leo katika Kongamano la Kwanza la Maendeleo ya Sekta ya Habari, Dar es Salaam.

Kutokana na hali hiyo, Balile ametoa rai kwa Serikali kuhakikisha Uhuru wa habari unalindwa kwa mujibu wa Sheria.

"Tunaamini Serikali italinda Uhuru huu kisheria katika mabadiliko ya Sheria ya Habari yajayo," amesema. 
Balile amesema wadau wa habari wana matarajio makubwa kwamba ifikapo Januari, 2023 mapendekezo juu ya mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari yatawasilishwa Bungeni, kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.

“Nimezungumza na Waziri Nape {Nnauye}, amesema Januari {2023} mapendekezo yatafikishwa bungeni,” amebainisha.

Pamoja na hayo, Mwenyekiti huyo wa TEF amesema bado zipo taasisi za Serikali ikiwamo halmashauri ambazo hazijalipa madeni ambayo vyombo vya habari vinawadai.
“Mpaka mwishoni mwa mwaka jana, madeni ambayo vyombo vya habari vinadai kwa serikali na taasisi zake ni Tsh. 7 bilioni," amesema na kuongeza...

"Ukijumuisha na deni la Gazeti la Daily News la serikali {Tsh. 11 Bilioni}, jumla ya deni ni Tsh. 18 Bilioni na zaidi.

“Halmashauri wana roho ngumu, hawajalipa mpaka leo licha ya kuandikiwa barua na TAMISEMI. Tunaomba mheshimiwa waziri {Nape} liwekee mguu chini, utusaidie.

Picha kwa hisani ya John Bukuku

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement