Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Dar es Salaam 

Wizara ya Afya imekua mshindi wa kwanza miongoni mwa Wizara kumi ambazo zilichaguliwa na kushindanishwa kwa kutoa taarifa za Serikali kwa umma.

Tuzo hiyo imetolewa leo tarehe 18 Disemba 2022 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye katika kongamano la Maendeleo ya Sekta ya habari mwaka 2022 lililofanyika Jijini Dar Es Salaam.

Kongamano hilo limeshirikisha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Wizara, taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, Wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja na wadau wa sekta ya habari wa ndani na nje ya nchi.

Hii ni tuzo ya pili kwa Wizara ya Afya kupitia Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  baada ya mwezi Februari 2022 kupata tuzo ya mshindi wa kwanza upande wa Wizara kutoka Tanzania Digital Award iliyotambua mchango wa Wizara kuhabarisha umma kupitia mitandao ya kijamii.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement