Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Dawa tiba aina ya 'Pethidine' yenye asili ya kulevya imekamatwa ikiuzwa kinyume cha Sheria kwa usiri mkubwa kwa wananchi mitaani, kupitia maduka ya dawa muhimu, Tanzania.

Oparesheni maalum ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba [TMDA] iliyofanywa kipindi cha Novemba 20 hadi 24, 2023, imeibua hilo.

TMDA imefanya oparesheni hiyo ikishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya [DCEA], Baraza la Famasi na Jeshi la Polisi Tanzania.

"Dawa zenye madhara ya kulevya aina ya Pethidine nazo zimekamatwa zikiuzwa kwa siri, mtandao wote umebainika  na wahusika kufahamika," amesema Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo.

Ameongeza "Haziruhusiwi kuwa kwenye soko [mitaani], zina utaratibu wake ni 'controlled' [usimamizi mkali].

"Zinatakiwa kuwepo hospitali tu na kwa ruhusa maalum, hazipaswi kuwa nje ya utaratibu mtaani [kwani hutumika kwa matibabu maalum tu]," amesema.

Akimwakilisha Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo, Kamishna wa Ukaguzi na Sayansi Jinai wa DCEA Dominic Mutayoba amesema kazi kubwa imefanyika.

"DCEA kazi yetu kubwa ni kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya,," amesema na kuongeza,

"Tunafanya kazi na kufuatilia kwa ukaribu dawa tiba zenye asili ya kulevya zisichepushwe na kutumiwa kama dawa za kulevya kwa kushirikiana na Mamlaka zote za Udhibiti.

"Lakini pamoja na jitihada kubwa zinazoendelea bado wapo watu wachache wanaokiuka sheria na miongozo iliyopo ya udhibiti na kupelekea upatikanaji holela wa dawa hizo.

Amesema hali hiyo inachochea matumizi ya dawa tiba zenye asili ya kulevya, dawa hizo zinatumika kiholela kwa baadhi ya maeneo bila kufuata miongozo.

"Kuchanganywa dawa tiba na zingine zenye asili ya kulevya, kwenye vinywaji kupitia shisha na hata bangi.

"[Yaani kadri] tunavyoongeza jitihada za kudhibiti dawa nyingine zinazoingizwa nchini kutoka nje huku tunapata mwaya wa wengine kujiingiza katika matumizi ya dawa tiba zenye asili ya kulevya.

"Unaweza kuona kazi si ndogo, kazi ni kubwa... tunashirikiana na Mamlaka zote kuhakikisha hili haliongezeki na kuwa tatizo kubwa.

Ameongeza "Nitoe wito kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa DCEA, hakuna eneo tutakaloliacha lipumue na kuchochea ongezeko la matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya.

"Kupitia dawa tiba zenye asili ya kulevya, kuanzia dawa za mashambani, za viwandani na kemikali bashirifu zinazoweza kupelekea matumizi ya dawa za kulevya," amesema.

Ameiomba jamii iendelee kushirikiana na DCEA kufichua wale wasio na nia njema wanaojihusisha na biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini.

TMDA ilifanya oparesheni hiyo kwenye wilaya mbalimbali katika mikoa 13 ikiwamo Dar es Salaam, Dodoma, Mbeya, Songwe, Lindi na Ruvuma.

Wilaya au Mikoa husika ilichaguliwa kutokana na rekodi za matokeo ya miaka ya nyuma ya kaguzi zake mbalimbali pia taarifa za kiintelijensia kutoka vyombo vya udhibiti nchini.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement