Na Veronica Mrema
Idadi
ya watoto 5,410,576 walio chini ya umri wa miaka mitano sawa na 38.8% walipata
magonjwa ya maambukizi katika mfumo wa hewa wa juu kwa mfano mafua na kikohozi
katika mwaka 2023.
Waziri
wa Afya Ummy Mwalimu amesema hayo leo alipotoa taarifa kwa Umma kuhusu hali ya
kwa mwaka 2023 na kutaja vipaumbele vya Wizara hiyo kwa mwaka 2024.
Ametaja
magonjwa mengine yaliyotesa kundi hilo ni malaria ambapo waliougua walikuwa 1,483,846
[10.7%], kuharisha bila upungufu wa maji watoto 1,68,763 [8.4%].
“Maambukizi
katika njia ya mkojo [UTI] watoto 1,050,723 [7.5%], Homa ya Mapafu [Nimonia] 1,029,548
[7.4%].
“Maambukizi
ya Ngozi [yasiyo fangasi] watoto 526,983 [3.8%], magonjwa mengineyo ya mfumo wa
chakula yasiyo ya kuambukiza 524,698 [3.8%].
Ametaja
magonjwa mengine ni ya minyoo watoto 402,425 [2.9%], kuharisha na upungufu wa maji
319,686 [2.3%] na maambukizi ya ngozi [fangasi] watoto 308,353 [2.2%].
Kwa upande wa watu wenye umri wa miaka mitano na zaidi magonjwa 10 yaliyowatesa zaidi Watanzania ni maambukizi katika mfumo wa hewa wa juu wagonjwa 4,901,844 [18.9%].
“Maambukizi
katika njia ya mkojo [UTI] 4,095,104 [15.8%], malaria 1,772,523 [6.9%], shinikizo
la damu 1,455,165 [5.7%].
“Vidonda
vya tumbo 963,520 [3.7%], magonjwa mengineyo yasiyo ya kuambukiza 830,059 [3.2%],
homa ya mapafu [Nimonia] 703,666 [2.7%], kisukari 652,455 [2.5%].
Ametaja
magonjwa mengine ni ya minyoo 611,538 [2.4%] na magonjwa mchanganyiko 552,661 [2.1%].
“Tumeona ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza
kama shinikizo la damu kutoka 2.7% hadi 5.6% kwa mwaka 2023,” amesema na kusisitiza,
“Ugonjwa wa kisukari idadi
imeongezeka kutoka 1.6% hadi 2.5%. Amewahimiza Watanzania kuzingatia mtindo bora
wa maisha hususan ulaji unaofaa ili kuepuka magonjwa yasiyo ambukiza.
Chapisha Maoni