Na Veronica Mrema
‘Darasa’
la mtindo bora wa maisha hususan kuzingatia ulaji unaofaa linalotolewa mara kwa
mara kwa jamii na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili [MNH], ni zuri.
Siku
za hivi karibuni mafundisho yake yamejizolea umaarufu mkubwa na kuibua mijadala
mingi katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
Prof.
Janabi amekuwa akihimiza wanajamii kuepuka ulaji usiofaa ikiwamo vyakula vya
wanga kwa wingi, matumizi ya sukari nyingi na chumvi ya mezani ili kuepuka
magonjwa yasiyoambukiza.
Waziri
wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu hali ya
utoaji huduma za afya kwa mwaka 2023, amesema jamii haipaswi kupuuza mafundisho
ya Prof. Janabi.
“Mafundisho
yake hata mimi yananitisha lakini jamii isiyapuuze,” amedokeza na kuongeza,
"Watu wanafanya
mzaha na Prof. Janabi na mafundisho anayotoa, japo wakati mwingine hata mimi ananitisha.
“Lakini
mimi ni mwanafunzi wake na ‘ameniharibu’ [amenibadilisha] tangu Mei 2023 sinywi
chai yenye sukari,” amebainisha Waziri Ummy.
Prof. Janabi
kabla ya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa MNH amewahi kuiongoza Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete [JKCI] kwa takriban miaka saba, uhimiza jamii kuepuka pia unywaji wa pombe.
Amekuwa
akieleza madhara makubwa yatokanayo na mtindo mbovu wa maisha, ulaji usiofaa na
unywaji wa pombe unavyochangia magonjwa yasiyoambukiza.
Magonjwa
hayo katika ripoti yake, Waziri Ummy amesema ni kati ya magonjwa 10 yaliyoongoza
kwa idadi kubwa ya wagonjwa Tanzania, mwaka 2023 kundi la wenye miaka mitano na
zaidi.
Amebainisha
“Tumeona ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza
kama shinikizo la damu kutoka 2.7% hadi 5.6% kwa mwaka 2023.
“Ugonjwa wa kisukari idadi
imeongezeka kutoka 1.6% hadi 2.5%. Amewahimiza Watanzania kuzingatia mtindo
bora wa maisha hususan ulaji unaofaa ili kuepuka magonjwa yasiyo ambukiza.
Pamoja
na hayo, magonjwa ya maambukizi katika mfumo wa hewa wa juu imerekodiwa idadi ya
wagonjwa 4,901,844 [18.9%].
“Maambukizi
katika njia ya mkojo [UTI] 4,095,104 [15.8%], malaria 1,772,523 [6.9%],
shinikizo la damu 1,455,165 [5.7%].
“Vidonda
vya tumbo 963,520 [3.7%], magonjwa mengineyo yasiyo ya kuambukiza 830,059
[3.2%], homa ya mapafu [Nimonia] 703,666 [2.7%], kisukari 652,455 [2.5%].
Ametaja
magonjwa mengine ni ya minyoo 611,538 [2.4%] na magonjwa mchanganyiko 552,661
[2.1%].
Chapisha Maoni