Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Dar es Salaam

Kasi ya ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya ni ushindi mkubwa katika vita dhidi ya janga hilo kwa Taifa la Tanzania, hatua ambayo inastahili pongezi nyingi.

Mapema leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefanya ziara Makao Makuu ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya [DCEA] Dar es Salaam na kuwapa 'maua tele' [yaani] pongezi.

Ni siku chache tu tangu DCEA ilipokamata kiasi cha zaidi ya Tani 3 za dawa za kulevya mwishoni mwa Desemba, 2023.

Akizungumza na maafisa wa DCEA, PM majaliwa amesema Serikali inathamini kazi kubwa ambayo wanaoifanya katika kuokoa kizazi cha Tanzania.

‘‘Nimekuja kuona mwenyewe zile dawa mlizokamata... lakini pia kuwapongeza kwa kazi nzuri mliyoifanya," amesema na kuongeza,

"Mafanikio haya yanaanza kuleta sura ya kwamba Tanzania si mahali sahihi kwa kuzalisha, kusafirisha, kuuza na sio mahali pazuri kwa Matumizi ya Dawa za kulevya.

Ameitaka DCEA kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa nchini.

"Serikali  itaendelea kuiwezesha mamlaka hiyo ili iweze kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi," ameahidi.

Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo, amemshukuru PM Majaliwa na Serikali kwa ujumla, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka kufanikisha kazi zake.

‘‘Naomba kukushuru wewe Waziri Mkuu kwa kuendelea kuisimamia Mamlaka katika kutekeleza kazi zake vizuri chini ya maelekezo na maagizo yako unayoyatoa mara kwa mara kupitia wasaidizi wako.

Ameongeza ".., na sisi kama watumishi tunahakikisha tunatekeleza maagizo yako kwa weledi na ufanisi mkubwa, ili kuhakikisha malengo ya Tanzania bila dawa za kulevya inawezekana na kuwa salama.

Desemba, 2023 DCEA ilikamata dawa za kulevya zaidi ya tani 3 katika eneo la Kibada, Dar es Salaam.

Dawa hizo ni aina ya Heroin na Methamphetamine, kiwango cha dawa hizo za kulevya kilichokamatwa ni kikubwa ambacho hakijawahi kukamatwa nchini tangu shughuli za udhibiti zianze kufanyika nchini.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement