Na Veronica Mrema
Siku 69
za mapambano ya kudhibiti ugonjwa wa virusi vya Marburg ndani ya Mkoa wa Kagera,
zimeiandikia historia ya kipekee Tanzania, ulimwenguni.
Tanzania
ni nchi iliyoweza kukomesha ugonjwa huo kwa kipindi kifupi zaidi kuliko nchi nyingine
ambazo zimewahi kupata mlipuko.
Yameelezwa
hayo leo Dar es Salaam na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alipowasilisha taarifa ya
hali ya utoaji huduma za afya Tanzania kwa mwaka 2023 kwa waandishi wa habari.
“Kwa mwaka 2023, nchi yetu iliweza
kupambana na kudhibiti ugonjwa wa Marburg
Mkoa wa Kagera ambapo jumla ya Visa 9 na Vifo 6 vilitolewa taarifa,” amesema.
Ameongeza
“Wizara kwa kushirikiana na wizara nyingine pamoja na wadau wengine wa Afya ilifanikiwa
kudhibiti mlipuko ndani ya siku 69.
“Tofauti na nchi nyingine ambazo huchukua hadi miezi 6 kudhibiti milipuko kama hii.
Amesema katika kipindi hicho Wizara imeendelea kufuatilia mwenendo wa magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa.
“Maambukizi ya UVIKO 19 yaliongezeka nchini kutoka wastani wa visa 12 bila kifo kwa wiki kwa Mwezi Julai 2023 hadi wastani wa visa 21 bila kifo kwa wiki kwa mwezi Desemba, 2023.
Amesema Maambukizi ya Influenza yalikuwa 903 bila kifo kwa mwaka 2023, tulipata ugonjwa wa Kimeta mikoa ya Kilimanjaro, Songwe, Arusha na Rukwa.
“Idadi ya wagonjwa wa Kimeta walikuwa 76 na kifo 1,” amesema Waziri Ummy.
Amesema kwa upande wa ugonjwa wa kipindupindu Wizara ilitoa ripoti ya mikoa 12 ambapo wagonjwa 927 na vifo 27 vilitolewa taarifa.
“Mkoa wa Arusha uliongoza kwa visa 214 lakini bahati nzuri hakukutokea kifo, katika mkoa wa Mara jumla ya visa 193 na vifo vinane vilitolewa taarifa.
“Mkoa wa Simiyu Visa 184 na vifo viwili, mpaka sasa kuna mikoa 6 ambayo inaendelea na mlipuko, ambayo ni Shinyanga, Rvuma, Tabora, Simiyu, Mwanza na Kagera,” ameitaja.
Amesema
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu atatoa taarifa ya kina siku si nyingi
juu ya mwenendo wa ugonjwa huo.
Chapisha Maoni