Na Veronica Mrema
Idadi ya wagonjwa kutoka nje ya nchi
wanaofuata huduma za matibabu nchini Tanzania imezidi kuongezeka kutoka 5,705 mwaka
2022 hadi 6,931 mwaka 2023.
Ongezeko hilo ni kutokana na uwekezaji
mkubwa uliofanywa na Serikali wa uboreshaji huduma za kibingwa na bobezi.
Wagonjwa hawa wanatoka nchi za Comoro,
Malawi, Burundi, Zambia, Congo DRC, Uganda, Zimbabwe na Kenya,” amebainisha Waziri
wa Afya Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy alikuwa akitoa taarifa
ya Hali ya Utoaji Huduma kwa mwaka 2023 katika mkutano wake na waandishi wa habari,
mapema leo Dar es Salaam.
Ameongeza “Wagonjwa hawa
walihudumiwa katika hospitali 6 ikiwamo Hospitali ya Taifa Muhimbili [MNH], Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Amebainisha
hospitali nyingine ni Taasisi ya Mifupa MOI Aga Khan na Safee ambazo zenyewe ni
za sekta binafsi.
“Tanzania
imekuwa kimbilio la wagonjwa kutoka nje ya nchi, na wagonjwa hawa wanaleta
fedha za kigeni na hivyo kuchangia pato la Taifa,” amesema.
Amesisitiza
kwa upekee wa Kiuchumi na kijiografia wa Tanzania ikiwamo uanachama hai wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC, kuzungukwa na nchi nane na kuwa na Bahari ya Hindi,
.., kama
mpaka wake upande wote wa mashariki, kumeifanya kuwa “Lango la Afrika”.
“Kunatuweka
kwenye fursa adimu ya kuwa “Kitovu cha Tiba Utalii” katika ukanda wa Afrika Mashariki,
Kati na Kusini,” amesisitiza Waziri Ummy.
Chapisha Maoni