Picha kwa hisani ya mtandao.
Kila mwaka kuna wanawake wapatao milioni 2 ambao
hubeba ujauzito, jamii imeonekana kuwa na mwamko mzuri wa kuzingatia mahudhurio
manne ya kliniki, Tanzania.
Eneo la huduma za afya ya uzazi, mama na mtoto ni
kati ya yaliyofanyiwa tathmini na Wizara ya Afya kwa mwaka 2023 kwa kuzingatia
viashiria vikuu 16.
Miongoni mwa viashiria hivyo ni mahudhurio angalau
mara nne au zaidi [ANC Visit] kwa kundi hilo.
Moja ya kiashiria kikuu cha ubora wa huduma za afya
nchi yoyote duniani ni kuwa na kiwango cha wajawazito wanaojifungulia katika
vituo vya kutolea huduma za afya.
Ripoti ya Wizara ya Afya ya Hali ya Utoaji Huduma
kwa mwaka 2023 imeeleza kwa mwaka 2023 wajawazito
2,391,427 [97.5% walihudhuria Klinic mara nne katika kipindi cha ujauzito wao.
Hata hivyo idadi hiyo imetajwa
kushuka kidogo kulinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2022.
Ripoti hiyo imeeleza katika
mwaka huo wajawazito 2,442,580 [102%] walihudhuria kliniki mara nne katika
kipindi cha ujauzito wao.
Licha ya hali kuwa hivyo, bado
Tanzania ipo katika lengo iliyojiwekea kufikia 80% mwaka 2030 kama ambavyo pia
imeelekezwa na Shirika la Afya Duniani [WHO].
“Hii inaonesha, Watanzania wana mwamko mkubwa na wanatambua umuhimu wa
wajawazito kufanya mahudhuria ya kliniki wakati wa ujauzito ili kupata huduma
stahiki,”.
Ni kauli
yake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ambapo pia amesisitiza “Hili ni eneo ambalo nalipenda
na ndipo ulipo ‘moyo’ wa Rais Samia Suluhu Hassan.
“Tumepita
lengo lililowekwa na WHO pamoja na Mpango [wetu] Mkakati wa Kuimarisha Huduma za
Afya ya Mama na Mtoto [One Plan III],” amesema.
Ameongeza
“Mahudhurio ya kliniki yanaonesha wajawazito wana imani na huduma zinazotolewa na
wanatambua umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito ili kupata huduma sahihi.
Chapisha Maoni