Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Dar es Salaam

Soko la ndani, bidhaa za dawa Tanzania limefanyiwa ukaguzi wa kina na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba [TMDA], kufuatia iwapo dawa duni ya vidonge aina ya Fluconazole Milligram 200 ipo.

Dawa hiyo inazalishwa na kiwanda cha Universal Corporation kilichopo Kikuyu Kenya, imeripotiwa na nchi ya Rwanda kwamba ni duni.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo amesema Desemba 29, 2023 walipokea taarifa iliyotolewa na taasisi ya Udhibiti Chakula na Dawa nchini Rwanda [Rwanda FDA] juu ya uwepo katika soko la nchi hiyo.

Amebainisha taarifa hiyo ilieleza juu ya uwepo wa matoleo duni ya dawa aina ya Fluconazole ya vidonge ya miligramu 200 yaliyotengenezwa na kiwanda cha Universal Corporation kilichopo Kikuyu nchini Kenya katika Kitalu Na.13777, Club Road.
Ametaja matoleo duni ya dawa hiyo ni Na. 5810315, 5810316, 5811390 na 5810022 na kuisha muda wake wa matumizi, Agosti, 2025.

"RFDA imefanya hivyo ili kutekeleza matakwa ya Shirika la Afya Duniani [WHO] ya kutoa taarifa za uwepo wa dawa duni na bandia ili mamlaka zingine za udhibiti wa dawa duniani nazo ziweze kuchukua hatua iwapo matoleo husika yatakuwa yamesambazwa katika nchi zao," amesema.
Ameongeza "TMDA inapenda kuujulisha umma kuwa haijasajili dawa hiyo ya vidonge [Fluconazole 200mg tablets] badala yake imesajili dawa hiyo ikiwa katika mfumo wa kapsuli za miligramu 150 na 200 ([Fluconazole 150mgand 200mg Capsule] kutoka kiwanda hicho. 

"Aidha, tunapenda kuujulisha umma kuwa TMDA haijatoa kibali cha kuingiza dawa hiyo nchini. 

Amesema hata hivyo, kwa kuwa kuna uwezekano wa dawa hiyo kuingizwa nchini kwa njia haramu na mipaka isiyo rasmi.

"TMDA ilichukua hatua ya kufuatilia katika soko la nchi yetu na kujiridhisha kuwa matoleo tajwa ya dawa hiyo hayajaingizwa nchini," amesema.

Fimbo amesisitiza "Mamlaka itaendelea kufanya ufuatiliaji zaidi wa dawa zilizosajiliwa kutoka kiwanda hicho pamoja na viwanda vingine kwa lengo la kuendelea kulinda afya ya jamii.

 TMDA ni taasisi ya Serikali ilyo chini ya Wizara ya Afya iliyoanzishwa chini ya Kifungu cha4 [1] cha Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba Sura, 219. 

Mamlaka hiyo ina jukumu la kulinda afya ya jamii kwa kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement