Utoro ni zao la uhalifu, baadhi
ya watoto waliopo shuleni hujificha kwenye makorongo na maeneo mengine
mbalimbali ambako huko hutekwa na vijana wakubwa na kufanyiwa uhalifu.
Ikiwamo kuvutishwa bangi,
kubebeshwa au wao kulawitiwa hali hiyo imeifanya Jeshi la Polisi kuja na mbinu
ya kusaidia kuokoa kizazi cha Tanzania.
‘Pembe tatu’ madhubuti ni nyenzo iliyoundwa, inayotumika kuwaokoa/kuwapuesha watoto dhidi ya janga la
matumizi na biashara ya dawa za kulevya,
Askari A/INSP Verediana Milimba ambaye ni Mkaguzi
Msaidizi Wilaya ya Dodoma Mjini [Kitengo cha Ushirikishwaji Jamii - Polisi
Kata- Kata ya Hazina] anafafanua zaidi,
“Tumeweka mikakati mbalimbali ambayo kwa kiwango kikubwa inatusaidia kuifikia jamii," Askari A/INSP Verediana Milimba anafafanua.
Ni Mkaguzi Msaidizi Wilaya ya Dodoma Mjini [Kitengo cha Ushirikishwaji Jamii - Polisi Kata- Kata ya Hazina] anasema wanshirikia na DCEA [Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya].
“Sisi tumeweka mikakati
ambayo kwa kiasi kikubwa inatusaidia kufikia jamii kwa ujumla," anasema.
anabainisha Mkakati wa kwanza ni mradi wa
usalama wetu kwanza ambao umelenga zaidi watoto walioko ma-shuleni kuanzia
shule kuanzia ya msingi, sekondari na vyuo.
“Lengo kuu kwanza ni kudhibiti
utoto kwa sababu tumegundua ni zao la uhalifu wanajificha kwenye makorongo,
maeneo mbalimbali wanatekwa na vijana wakubwa kufanyiwa uhalifu.
“Ikiwamo kuvutishwa bangi, kubebeshwa
ama wao kulawitiwa,” anasema na kusisitiza,
“Kwa hiyo tulianza kwanza kukemea
[utoro], tulitengeneza ‘pembe-tatu’ kuanzia Polisi [askari], walimu, DCEA na
mzazi ili kudhibiti utoro.
“Halafu tunawapa elimu wao
kukataa kuwa wasambazaji kwa namna yoyote ile, kwa maana abebe mzigo kama mtu
amempatia ajue amebeba nini.
“.., na asipojua leo kabeba nini, kupeleka wapi, basi atoe taarifa kwa mwalimu rafiki kwa maana ya program rafiki za msingi au sekondari.
Anafafanua “.., kwamba leo
nimebeba kitu fulani, kupeleka sehemu fulani na sikijui, ili tuweze kufanya
ufuatiliaji alibeba nini na zaidi tunawaambia hata kwa kutokujua watoe taarifa.
Anasema wanashirikiana kwa ukaribu
na DCEA katika kutambua wajasiriamali wote wanaofanya biashara katika maeneo ya
shule.
“Shule zetu zimezungukwa na
wajasiriamali wengi ambazo hazina uzio, kwa hiyo unakuta kuna muingiliano
mkubwa kati ya watoto na raia.
“Tunachokifanya ni kuhakikisha
tunawatambua wajasiriamali wote ambao wapo ndani ya maeneo ya shule tunafanya
nao vikao na kuwapa elimu.
Anasisitiza “.., na tumetoa ombi
rasmi kwa wakuu wote wa shule kuwaomba wawatambue kwa vitambulisho ili kuepusha
wale wanaopita kwa njia kwamba wamepita ameuza akaondoka.
“Isije ikatokea wale wenye nia
ovu kuzalisha waraibu wapya katika rika la watoto, licha ya hivyo tunawapa
watoto pia elimu wajitahidi kununua vitu ambavyo viopo ndani ya mipaka ya
shule.
“Ambayo sisi tumejiridhisha hawa
wajasiriamali sisi tumeshawahihi na tumejiridhisha hawa tumeshawahihi na
tunafanya ufuatiliaji hata historia zao za nyuma,” anasema.
Anasema wanahamasisha watoto wasivuke
nje ya shule kwenda ng’ambo ya barabara ambapo si sehemu ya wale wajasiriamali waliotambuliwa.
Anasema wanahimizwa siende kufuata
bidhaa ili kuwaepusha kuwa waraibu kupitia zile bidhaa ambazo zinauzwa.
Juhudi za kuokoa kizazi cha
Tanzania haifanyiki ndani ya shule na vyuo pekee, DCEA imezidi kuongeza nguvu
ndani ya jamii kupambana na ‘mapapa wa unga’.
Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas
Lyimo anasema jamii imeendelea kupewa elimu kuhusu Sheria ya Kudhibiti na
Kupambana na Dawa za Kulevya namba 5 ya mwaka 2015.
Anasema Sheria hiyo inatoa adhabu
kali kwa makosa mbalimbali yanayohusiana na makosa ya dawa za kulevya.
“Ukikamatwa unajihusisha,
unasafirisha, unauza, unatumia. Sheria yetu inaweza kukufunga hadi kifungo cha
maisha gerezani,” anasema.
Anaongeza “Ndiyo maana tupo
katika wiki ya sheria kwa sababu mahakama ni mdau wetu mkubwa katika mnyororo
wa haki jinai.
“Tunashirikiana na mahakama na
taasisi zote za haki jinai kutoa elimu kwa wananchi ili wajiepushe na biashara
ya dawa za kulevya.
Anasema katika oparesheni mbalimbali
wanazozifanya tumebaini watoto wengi hasa wale wanaoacha shule, wanaotelekezwa
mitaani ndiyo wengi wanaotumika.
“…, katika usafirishaji wa dawa
za kulevya katika maeneo mbalimbali,” anasema na kuongeza,
“Watu wanatumia nafasi hizo kwa
wale watoto katika kuwatumia kumeza dawa za kulevya na kusafirisha maeneo
mbalimbaliu.
“Wengine wanawatumia kusafirisha
maeneo mbalimbali kutokana na kwamba wakiamini wale watoto hawawezi
wakagundulika mapema.
Anasema baada ya kubaini hilo
sasa DCEA inashirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanatoa elimu vijijini, mijini
[mitaani], familia kwa familia kuhimiza wazazi kulea vema watoto wao.
“Wazazi watambue tabia za watoto
wao mapema ili wasishiriki katika tabia hiyo [isiyofaa] ili pia wahakikishe
wanalinda watoto wao .
“.., wasije wakatumika katika
kusafirisha dawa za kulevya kwa sababu katika kushiriki kumeza wakati mwingine
ukimeza lazima uonje kidogo dawa za kulevya.
“Ili uweze kumudu kubeba kwa muda
mrefu, mwisho wake unajikuta yule mtoto anayetumika katika kubeba dawa za
kulevya naye anakuwa mtumiaji, mraibu wa dawa za kulevya.
Anaongeza “Unakuta tatizo la dawa
za kulevya linaendelea, tutoe rai wazazi, viongozi wa dini, familia na jamii
kwa ujumla tushirikiane watoto wasiingie katika matumizi ya dawa za kulevya.
ORODHA YA 'RIMOTI'
Anasema DCEA inaendelea kubaini
mitandao ya ‘mapapa wa unga’ wanaojihusisha na biashara haramu ya cocaine,
heroin na metamphetamine.
Kamishna Jenerali Lyimo anasema wanaendelea
kubaini pia hadi mtandao wa wakulima wakubwa wa dawa za kulevya za mashambani
ikiwamo bangi na mirungi.
“Orodha tuliyonayo sasa hivi
tumebaini wengi wanafanya biashara hii kwa ‘rimoti’ [yaani] wapo lakini hawafanyi
[waziwazi].
“Wanawatumia watu, tumeshawatambua
[‘mapapa’ hao] tunayo orodha na wale wanaofanya [kwa ‘rimoti’] tunayo.
Anasisitiza “Tutawaunganisha na
tunajua na wengine wana biashara zao kubwa tu [zisizo za ‘unga’/wamejificha
humo].
“Tuwaonye waache hiyo biashara
tutawakamata na mwisho wa siku watadhalilika, waache biashara hiyo [ya ‘unga’].
“.., watafute biashara halali za
kufanya ili tujenge Taifa letu, uchumi wetu na ustawi wa jamii tuhakikishe
biashara ya dawa za kulevya inaisha,” anaesisitiza.
Chapisha Maoni