Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Mkurugenzi ORCI aeleza akili bandia, ‘proton therapy’ zitakavyosaidia

Na Veronica Mrema

Teknolojia za viwango vya juu na za kisasa zaidi katika uchunguzi na tiba dhidi ya magonjwa ya saratani, zitakazosimikwa ndani ya Kituo cha Umahiri wa Matibabu ya Saratani Afrika zitainua zaidi Tiba Utalii, Tanzania.

Taasisi ya Global Health Catalyst ya Marekani imedhamiria kujenga kituo hicho cha kisasa Tanzania huko Dodoma kwa ajili ya kutoa huduma zake kwa Bara la Afrika.

Februari 6, 2024 uongozi wa GHC ulisaini makubaliano [MoU] na Wizara ya Afya Tanzania kwa ajili ya kituo hicho na tayari umeanza kukusanya fedha kufanikisha ujenzi.

Ndani ya kituo hicho kutasimikwa teknolojia za kisasa sawa na zile zinazotumika nchi zilizoendelea ikiwamo Marekani yenyewe katika kuchunguza na kutibu magonjwa hayo.

Ikiwamo teknolojia ya akili bandia/mnemba [Artificial Intelligence] na tiba ya ‘Proton Therapy’.

Akizungumza na MATUKIO NA MAISHA BLOG katika mahojiano maalum, Mratibu wa Tiba Utalii Wizara ya Afya, Dkt. Asha Mahita amesema Tanzania itapiga hatua kubwa Barani Afrika.

“Kutokana na fursa ambayo tumeipata kupitia Global Cataltyst ambayo sasa inafanya ‘fund rising’ kuhakikisha tunaweza kujenga kito cha matibabu ya saratani cha mfano nchini,” amesema.

Dkt. Mahita ameongeza “Kituo hicho kitakuwa kinafanya utafiti, kinavumbua matatizo ya saratani, kinatoa matibabu kikiwepo Tanzania kitatusaidia sana katika kuimarisha huduma za tiba utalii.

“Kwa sababu itatutangazia Tanzania tumekuwa based kwa masuala ya saratanibhususan kwenye nchi za Afrika.

“Ni fursa kubwa sana kama nchi, itapokea wagonjwa kutoka nchi mbalimbali watakaokuja kutibiwa saratani,” amesisitiza.

Amesema hivi sasa Tanzania inapokea wagonjwa wa saratani wanaofuata huduma za uchunguzi na tiba kutoka nchi mbalimbali Afrika.

“Tunapokea wagonjwa kutoka Malawi, Zambia, komoro wanapatiwa matibabu Taaisisi ya Saratani Ocean Road [ORCI] na hospitali binafsi ikiwamo Aghakhan na Saiffee, Bugando na KCMC.

Ameongeza “[Hivyo], uwepo wa kituo hiki itaiongezea nchi sifa kubwa kwamba tunaweza kufanya huduma za tiba utalii nchini.

MATUKIO NA MAISHA BLOG imezungumza pia na Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI Dkt. Julius Mwaiselage ambaye ameeleza namna ambavyo akili bandia itakavyotumika na kusaidia.

Amesema kufikia MoU ni hatua kubwa kwani kwa mwaka mmoja wamekuwa wakijadiliana na wawekezaji hao kuhusu ujenzi wa kituo hicho.

“‘Tanzania US regional advanced cancer treatment’ ni mwendelezo wa jitihada ambazo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akizifanya baada ya kukutana na wadau katika mkutano wa AfrikaUS.

Ameongeza “Aliwaomba wadau kutoka Marekani waje kuwekeza Tanzania tulikuwa nao kwa muda wa mwaka mmoja kujadiliana. 

“Wamekuja kusaini mkataba kuonesha ‘commintment’ yao [utayari wao] na tayari wamepata kiasi cha Dola mil 30 kama Tsh. Bil. 75, [kikao hicho] mgeni rasmi alikuwa Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

“Kumetokea ahadi mbalimbali kutoa kwa wadau, mashine ya kisasa Dola mil 20 inagharimu dola kama mil. 25 kati ya zile 30 tunazotaka. 

Amefaanua kituo kitakuwa na maeneo makubwa manne, huduma za kinga na kwenda mikoani kugundua saratani mapema, huduma za saratani katkia ‘cloud’. 

“Itakuwa rahisi kuwasiliana na wenzetu Marekani kiteknolojia,” amebainisha.

Amesema mafunzo na utafiti itakuwa ni sawa na huduma za saratani zilizokuwapo marekani, ndiyo maana umeona wengi wamekuja hapa kuhakikisha kikamilike.

Amesema kituo hicho kinatarajiwa kuwa kimejengwa na kukamilika ndani ya miaka mitano kuanzia sasa.

“Tutakuwa na kituo cha umahiri katika huduma za saratani kitatoa afrika mashariki na kati kusini mwa jangwa la sahara. 

“Kwa jinsi teknolojia inavyokwenda mbele kuna huduma zinakuwa za kibingwa sana na kama nchi yako hakuna wataalamu basi huduma hizi za akili bandia ndizo zitatumika. 

Ameongeza “Ttutakuwa tutatuma taarifa za wagonjwa marekani watatusaidia kuangalia na kuona jinsi gani tutaweza kuwatibu vizuri. 

“Vipimo tutavituma na itatusaidia kutupa taarifa jinsi gani kwa uzuri zaidi,” amesema. 

Amesisitiza [akili bandia] ni eneo ambalo Tanzania itakuwa imeendelea kiviwango [advanced] kwa sababu huduma za namna hiyo ndizo zinazopatikana Marekani zitakuwa Tanzania. 

“Tuna upungfu wa watumishi ,kwenye eneo hili tulilo na upungufu tutatuma taarifa halafu akili bandia itatusidia katika kutengeneza ‘plan’.

“Kusoma picha na taarifa mbalimbali ili kutuma majibu kwa daktari kuendela na tiba ili hata kama mtaalamu hayupo itatusaidia daktari aendelee na tiba,” amesema. 

Saratani ipo katika kundi la magonjwa yasiyoambukiza ambayo hivi sasa inatesa mamilioni ya watu duniani.

Utafiti wa hivi karibuni wa Lancet unaonesha katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara mzigo wa saratani ni mkubwa na huenda utaongezeka maradufu ifikapo 2030. 

Kulingana na ripoti hiyo vifo vitokanavyo na saratani katika ukanda huu vitaongezeka maradufu kutoka 500,000 hadi Milioni moja. 

“Hatuwezi tukafumba macho.., mzigo wa saratani tukiangalia Tanzania tuna wagonjwa wapya wa saratani takriban 40,000 kila mwaka,” amesema Waziri wa Afya Ummy Mwalimu. 

Ameongeza “Kila mwaka vifo ni 26,000 … wanaokufa wengi kwa saratani Tanzania ni watu maskini, wa kipato cha chini. 

Amesema pamoja na kwamba takwimu za dunia zinaonesha Tanzania kuna wagonjwa wapya 40,000 lakini wanaofika hospitalini kwa mwaka ni takriban 30% tu. 

“Wagonjwa wengi wa saratani wapo majumbani, katika vijiji vyetu, mitaa yetu wanashindwa kufika katika vituo vya kutoa huduma za afya kwa sababu ya umbali. 

“Kwa sababu ya huduma kuwa ghali, lakini katika hawa wanaofika hospitalini habari mbaya 80% wanafika saratani ikiwa hatua ya 3 au 4 . 

“Kwa hiyo inakuwa ngumu kutibika na changamoto ya kupata matokeo mazuri ya tiba,” amesema. 

Amesisitiza “Hivyo, suala la saratani kwa Tanzania si tu suala la kutibu bali pia katika kuzuia, kudhibiti na kuhimiza watu kupata huduma. 

Amebainisha aina za saratani zinazowatesa zaidi Watanzania 25% ni ya kizazi, 10% ya matiti, 9% ya tezidume, 6.5% ya umio la chakula, 5.8% ya utumbo mpana na saratani nyinginezo.

“Saratani Tanzania inawakumba zaidi wanawake, hata ukienda Ocean Road wengi utawakuta ni wanawake,” amebainisha.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement