Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Visa vya baadhi ya watu ambao wamepata vidonda katika mboni ya jicho kutokana na matumizi holela ya dawa za macho walizotumika kujitibu binafsi tatizo la macho mekundu 'red eyes', vimeanza kurekodiwa Tanzania.

Wizara ya Afya hii leo imetoa tamko kuisisitiza jamii kuacha matumizi holela ya dawa za macho kwani yanaweza kusababisha upofu usiotibika.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya Prof. Paschal Ruggajo mbele ya wanahabari amezungumza hii leo.

Amesema matumizi holela ya dawa za kutibu macho inaweza kufanya wengi kupata madhara katika kioo cha jicho.

"Wananchi waache tabia ya kutumia dawa za macho kwa lengo la kutibu ugonjwa wa ‘Red Eyes’ zisizo rasmi kwani matumizi hayo yanaweza kupelekea upofu usiotibika," amesema.

Ameongeza "Kama ambavyo itakuwa kwa wengi wa wagonjwa waliokwisha kupata madhara kwenye kioo cha jicho kwa kutumia vitu hivyo.

Amesema ugonjwa wa ‘Red Eyes’ hauleti upofu lakini matumizi ya dawa zisizo rasmi na zinazonunuliwa kiholela yanaweza kupelekea upofu usiotibika.

Baadhi ya vitu ambavyo watu wamekuwa wakivitumia holela kujitibu tatizo hilo ni pamoja na dawa zenye vichocheo vya ‘steroids’.

"Wanajinunulia wenyewe kwenye maduka ya dawa, tangawizi, chai ya rangi illiyokolea majani, mafuta tete yaliyokuwa yakitumika wakati wa janga la Covid - 19, maji ya chumvi na maziwa ya mama, ambavyo vitu vyote hivyo sio salama na havijaelekezwa na wataalamu. 

Kulingana na takwimu za Wizara ya Afya tangu kuripotiwa kwa mlipuko wa ugonjwa huo hadi sasa takwimu zinaonesha ongezeko la kuenea la  ugonjwa.

 Jumla ya wagonjwa 12,332 wameonwa katika vituo vyetu vya tiba na wagonjwa hawa wameonwa katika Mikoa 23 ya Tanzania Bara.

Mikoa inayoongoza kwa ugonjwa huo ni Dar es Salaam wagonjwa 6,412, Pwani wagonjwa 4,041, Dodoma 363, Morogoro 307, Mtwara 193, Shinyanga 193, Tanga 190, Lindi 101.

Mikoa mingine ni Katavi ina jumla ya wagonjwa 94, Njombe 81, Ruvuma 77, Arusha 42, Mwanza 40, Mbeya 37, Songwe 33, Rukwa 31, Kilimanjaro 31, Geita 18, Singida 17, Kigoma 13, Simiyu 9, Mara 5 pamoja na Tabora 4.

Jamii imehimizwa kuzidu kuchukua hatua kuzuia kuenea kwa maambukizi ikiwamo kuzingatia usafi binafsi na kanuni za Afya.

Usafi wa mikono na uso, Kuzuia kugusa macho yako kadri uwezavyo.

" Nawa mikono na maji tiririka na sabuni au na tumia vipukusi mara kwa mara, zingatia kutokushikana mikono maeneo ya sehemu za ibada.

"Tumia taulo au leso za karatasi kufuta tongotongo au machozi, Fika Kwenye kituo cha kutolea huduma mara upatapo dalili hizi," amehimiza.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement