moja

Responsive Advertisement

Dodoma

Sekta ya afya nchini Tanzania itaendelea 'kuvuna' ujuzi' kwa kubadilisha teknolojia za mafunzo na elimu kwa ushirikiano na Serikali ya Misri.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu mapema leo amekutana na Balozi wa Misri nchini Tanzania Mhe. Sherif Abdelhamid Ismail kwa kikao chao cha kwanza, jijini hapa.

"Tutaendelea kubadilishana madaktari, wauguzi, mafundi wa radiolojia, mafundi maabara pamoja na wanasayansi wa tiba," amesema.

Pamoja na hayo, amemuomba Balozi huyo kusaidia wahudumu wa Afya ya Jamii [CHWs] watakaoajiriwa 137,000 wenye jukumu muhimu la kutoa huduma za Afya kwa watu ambao hawajafikiwa.  

“Chini ya utaratibu huu, itaashiria uwekezaji mkubwa wa rasilimali watu na uwezeshaji wa jamii ili kufikia lengo hili," amesema na kuongeza,

"Ushirikiano ni muhimu kuweza kukusanya rasilimali kutoka kwa washirika na kutumia miundombinu na mitandao iliyopo," amesisitiza.
Serikali ya Tanzania na Misri ziliingia mkataba wa makubaliano [MoU] kati ya Wizara ya Afya na Shirika la ALAMEDA Healthcare Group Oktoba, 2022.

Unalenga kushirikiana katika nyanja ya afya hasa upande wa huduma za kimatibabu kwa kubadilishana uzoefu, usimamizi wa hospitali na matibabu ya wagonjwa wa Kimataifa.

Balozi za Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Nchini Tanzania Sherif Abdelhamid Ismail amemshukuru Waziri Mwalimu kwa kumkaribisha na kufanya kikao hicho.

Balozi Ismail amemuahidi Waziri Ummy kwamba ataendelea vema ushirikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili, yaliyopo katika sekta ya afya.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement