Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Pengo bado lipo katika kuyakabili Magonjwa Yasiyoambukiza [NCD’s] Barani Afrika hali ambayo sasa inawaleta pamoja wanasayansi, watafiti, watunga Sera na wadau wa maendeleo kujadili kwa pamoja.

Washiriki zaidi ya 300 kutoka mataifa mbalimbali wapo nchini Tanzania kwa mkutano wa siku tatu [April 23 hadi 25, 2024] wakiangazia janga la NCD’s ili kuja na mkakati madhubuti wa pamoja kuyatokomeza.

Akizungumza na waandishi wa habari Dkt. Benido Impouma katika Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kujadili Namna ya kukabiliana na Magonjwa Yasiyoambukiza Afrika [ICPPA] kupitia PEN-Plus.

Tunaangalia namna ya kuyadhibiti [ICPPA] ni mpango/mkakati wa Afrika, tunalenga kutokomeza au kupunguza NCD’s angalau kwa 90% na zaidi.

Ameongeza “Ni kama ambavyo tumefanya kwenye ugonjwa wa Polio, ili kufikia lengo la kutokomeza NCD’s ni lazima [mataifa] kufanya kazi hii kwa pamoja,” amesema.

“Hivyo, kufikia huko tunafanya kazi bega kwa bega na Serikali ili mawaziri waweze kuonesha namna mkakati huu unaweza kufanyika.

Amesema mkakati huo utatekelezwa kivitendo kwa ngazi ya Kimataifa na watafuatilia nchi kwa nchi.

“Tunajua kuna magonjwa mengi [ya NCD’s] yanayotesa Waafrika ikiwamo Siko Seli, kisukari na mengineyo.

“Tunapaswa kuyadhibiti na kila nchi inapaswa kufanya ili kuyadhibiti katika nchi husika.

Ameongeza “Si tu kupigania kuzuia ila tunapaswa kuwa na vitendea kazi [vifaa tiba vya kutosha] na kuweza kukusanya rasilimali [fedha] zitakazoweza kusaidia.

Amesema ndiyo maana mkutano huo unahusisha wadau muhimu ikiwamo Shirika la Afya Duniani [WHO],

Wadau na who kwa msaada tunaoupata na NCDI kwa ajili ya Mpango huu kuifikia malengo yake Kwa ukubwa zaidi.

Ofisa Program wa Helmsley Charitable Trusts Type 1 Diabetes [T1D] James Reid amesema walichogundua magonjwa mengi [ya NCD’s] huwaathiri pia watoto wadogo.

“Hasa Siko Seli na Kisukari hususan katika nchi zinazoendelea kulingana na tafiti za kisayansi.

“Hivyo, tulianza na kundi maalum kwa nchi zilizoanza utekelezaji wa mipango mingine iliyopo.

Amesema wameweza kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya kupitia WHO na wameona matokeo mazuri katika kuimarishwa kwa sekta ya afya kwenye nchi zao.

“Tunaona matokeo mazuri na mwanzo mzuri tunaamini itasaidia kupunguza vifo na kuokoa uhai zaidi.

Ameongeza “Tunajaribu kuangalia kwa watoto zaidi WHO inasaidia katika NCD's na kuna mfumo inatumika. 

“Kuna juhudi zinafanyika katika kuzuia magonjwa haya na kuhakikisha Pen Plus inaweza kusaidia kwa mfano Malawi.

“Nimeona wadau wanafanya nao kazi ikiwamo UNICEF na kuna huduma jumuishi za pamoja kufikia wananchi.

Amesisitiza “Tumefikia pazuri namna tutatoka hatua moja hadi nyingine tumepiga hatua kubwa Africa CDC na wengine wote wanaohakokisha tunatokomeza kisukari kwa mfuko.maalum.

Kwa pamoja wamepongeza hatua na juhudi za Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika mipango yake iliyoweka dhidi ya NCD’s.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement