Na Veronica Mrema
Utekelezaji mzuri wa kitita cha PEN-Plus kwa wenye Magonjwa
Yasiyoambukiza [NCD’s], Halmashauri ya Kondoa na Halmashauri ya Katavi, umeipa
heshima kubwa Tanzania Barani Afrika.
Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kutekeleza vema PEN-Plus
hatua ambayo imeipa fursa ya kuzipa somo nchi nyingine Barani humo ili kuongeza
nguvu ya mapambano dhidi ya NCD’s.
Ni kwa mantiki hiyo imekuwa mwenyeji wa Mkutano wa kwanza
wa Kimataifa wa Kujadili Namna ya Kukabiliana na NCD’s Barani Afrika ili
kufikia Malengo Endelevu ya Duniani [SDG’s].
“Jambo zuri wote [Afrika] tuna nia moja ya kupambana na NCD’s,
tumeona mtoto wa Tanzania [mgonjwa wa NCD’s aliyefikiwa na PEN-Plus] kwa muda
mrefu alishindwa kwenda shuleni.
“Lakini sasa ameweza kurudi shuleni,” amesema Mkuu wa Idara
ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa AfricaCDC Dkt. Mohammed Abdulaziz.
Dkt. Abdulaziz alikuwa akizungumza wakati wa hafla ya
ufungaji wa Mkutano wa Kujadili Namna ya Kukabiliana na Magonjwa
Yasiyoambukiza Barani Afrika [ICPPA].
Mkutano huo wa kwanza wa Kimataifa ulioratibiwa na Shirika
la Afya Duniani Kanda ya Afrika [AFRO-WHO] umefanyika April 23 hadi 25, 2024 Dar
es Salaam, Tanzania.
“Ni lazima tuweke mikakati bora ili kutatua changamoto za
ki-afya katika eneo la NCD’s, lazima tuwaangalie hawa wagonjwa wanahitaji
huduma sawia, uhakika wa matibabu na upatikanaji dawa.
Amesisitiza Dkt. Abdulaziz kwamba ni muhimu mapambano dhidi
ya NCD’s yakahusisha jamii moja kwa moja kwa kuipa elimu sahihi ili kuondosha
unyanyapaa kwa wale wanaougua.
“Tunahitaji kuendelea kuangazia haya na AfricaCDC tupo
tayari kuunga mkono ili kufikia lengo na kupata matokeo chanya,” amesema.
PEN-Plus ni kitita maalum cha huduma muhimu anazopewa mtu
mwenye ugonjwa usioambukiza katika vituo vya afya vya msingi [Primary Health
Facilities].
“Kwa pamoja Afrika tuna mkakati wetu na tulikutana kuweka
mikakati yetu kwamba tunakwenda ili kuweza kupambana na NCD’s,”.
Ni kauli yake Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Tanzania
Dkt. Hemed Nyenbea alipomwakilisha Waziri wa Afya Ummy Mwalimu katika kufunga
mkutano huo.
Ameongeza, “Lakini pia tulikuwa tukitekeleza [mkakati] kuendana
na malengo ya dunia [Endelevu – SDG’s].
“.., ambayo yaliwekwa ili kupunguza vifo vitokanavyo na NCD’s
angalau kufikia 25% ifikapo 2030,” amebainisha.
Amesisitiza ni mkutano wa kwanza wa aina yake kufanyika
Afrika ukiwa na agenda ya kupambana na NCD’s
“[Kimsingi] mapambano dhidi ya NCD’s yameanza muda mrefu
kidogo Afrika.., ila ni namna gani tuje pamoja kuweza kuweka mikakati, wamekuja
Tanzania.
“Tanzania imekuwa ndiyo nchi ya kwanza kuanza kutekeleza
vema mkakati huu,” amebainisha.
Ameongeza “Tulianza na PEN ilikuwa kitita cha huduma muhimu
kwa wenye NCD’s katika ngazi ya msingi [Halmashauri hadi zahanati] tulifanya
vizuri kwa kaisi kikubwa.
“Ilionekana haitoshi kuna watu wanaumwa sana mpaka wanapata
changamoto nyingi na kuhitaji rufaa kwenda hospitali kubwa.
“Ikaonekana kuna haja ya kupeleka hizi huduma mpaka kule
chini kabisa wlaipo wananchi ndiyo tunaita PEN-Plus.
Amesisitiza “Tumetekeleza Halmashauri mbili Kondoa na
Karatu mpaka wengine [kutoka nchi nyingine za Afrika] wamekuja kujifunza.
“WHO ikaona Tanzania ni nchi sahihi kabisa kufanya
kongamano la kwanza, ndiyo maana tumelileta hapa wamefurahia, wamejifunza
wamekuja hadi kutuuliza.
“Mpaka namna takwimu zetu zinavyopatikana tumewaeleza, lengo
la Serikali ni kuhakikisha mkakati huu unakwenda nchi nzima,
Amebainisha “Kama tunavyojua wananchi wengi wanapata huduma
ngazi za msingi, 80% wanaenda huko kwa sababu ndiyo za kwao na wanaenda kule na
wagonjwa wengi wapo kule.
“Ili kuweka usawa na kupunguza gharama kwa wananchi lengo
ni kupeleka hizi huduma ngazi za msingi, halmashauri zote, vituo vya afya na
hospitali ambako ndiko kuna wananchi wengi,”.
Chapisha Maoni