Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Mtu mmoja kwa mwaka alikuwa anakunywa lita 9.1 mwaka 2016 nchini Tanzania lakini sasa kiwango kimeongezeka maradufu hadi lita 10.4.

Hali hii inatajwa kuwa ni tishio jipya kwa afya za watu wanaojihusisha na unywaji huo wa pombe kali kupita kiasi, wanajiweka kwenye uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa yasiyoambukiza [NCD’s] .

Magonjwa hayo ni pamoja na yale ya moyo, kisukari, figo, shinikizo la damu na mengineyo ambayo sasa yanagharimu uhai wa mamilioni ya watu duniani hususan kundi la vijana.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amebainisha hilo leo alipokuwa akifungua Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kujadili Namna ya Kukabiliana na Magonjwa Yasiyoambukiza Barani Afrika [ICPPA].

Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu [April 23 hadi 25, 2024] Dar es Salaam ukiwa na washiriki zaidi ya 300 kutoka mataifa mbalimbali duniani.

“Magonjwa haya [NCD’s] kwa kiwango kikubwa yanatokana na mtindo mbovu wa maisha, ikiwamo unywaji pombe uliokithiri,” amesema.

Ameongeza “Tanzania tunaona ongezeko la unywaji wa pombe uliokithiri kuna kiwango kikubwa cha unywaji pombe kali [kupita kiasi].

“Tumepunguza watu wanaokunywa pombe tulikuwa na watu wanaokunywa pombe 26% mwaka 2016 [idadi] imeshuka hadi 20%.

“Lakini kiwango cha pombe imeongezeka kutoka 9.1 lita kwa mwaka hadi 10.4,” amebainisha.

Amewahimiza vijana kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya ikiwamo kupunguza unywaji wa pombe kupita kiasi,

“Tunahimiza watu wapunguze [unywaji pombe kupita kiasi] na tutaendelea kuhamasisha watu wafanye mazoezi [ya mwili].

“Nahimiza vijana [kufanya mazoezi ya mwili] tunao watu wazima wanafanya [hivi sasa].

Ameongeza “.., inawezekana wameshapata haya magonjwa yasiyoambukiza [ndiyo maana wamepata mwamko wa kufanya mazoezi].

“Vijana tusisubiri tupate [magonjwa haya ndipo] tufanye mazoezi,” amesema.

Amesisitiza “Unatoka nyumbani unapanda bodaboda.., unafika ofisini unakaa..,, unarudi nyumbani unakaa unaangalia runinga.., unakula.., unaenda kulala.

“[Mazoezi] si lazima ukimbie unaweza kutembea wataalamu wanasema angalau hatua 10,000 kwa siku.

“Jingine ni kuhamasisha wananchi kupima kwa sababu utambuzi wa mapema unafanya matibabu yanakuwa rahisi,” amesisitiza.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement