Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement

Na Veronica Mrema

Ukombozi wa afya ya mama na mtoto ni kipaumbele nambari moja na mahususi ndani ya Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania [MEWATA] ambapo imedhamiria kujenga hospitali kubwa ya kisasa.

'Well Women Center' [WWC] ni nia ya dhati inayolenga kuendeleza juhudi za Serikali ya kuimarisha afya ya mama, mtoto na jamii kwa ujumla nchini Tanzania.

Ujenzi wa WCC unatarajiwa kuanza mapema ndani ya mwaka huu ifikapo Desemba uzinduzi rasmi wa jiwe la msingi utafanyika, huko Mbweni Dar es Salaam kilipo kiwanja cha MEWATA.

Ni zaidi ya miaka 20 tangu MEWATA ilipoanzishwa nchini, imeweza kuibua wanawake 83,081 wenye saratani.., katika mikoa takriban 11 ambako walipita na kufanya uchunguzi wa awali wa magonjwa ya saratani.

Saratani hizo ni ile ya mlango/shingo ya kizazi na matiti ambazo kulingana na takwimu za Wizara ya Afya Tanzania ndizo zinazoongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu kila mwaka.

"Mikoa 11 [ikiwamo Dar es Salaam, Njombe, Mbeya, Manyara na Dodoma] tumeweza kuwapima saratani ya matiti wanawake 73,744 na wanawake 9,337 saratani ya mlango wa kizazi,".

Yamebainishwa hayo na  Rais wa MEWATA Dkt. Zaitun Bokhary mbele ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Mke wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Salma Kikwete huko Mbweni Dar es Salaam.

Ni katika kiwanja cha MEWATA itakapojengwa 'WWC' mapema leo yalipofanyika matembezi ya hisani [MEWATA WOGGING] .

"Katika uchunguzi wa awali tuligundua [wanawake] wengi wana matatizo mengi hususan magonjwa ya saratani [na] ilipelekea wengine kuripoti katika hatua za mwisho kabisa [3 na 4]," amesema.

Amesema kwa miaka mingi MEWATA imekuwa ikijitahidi mno katika kufanya uhamasishaji kwa jamii kuchunguza afya zao na kuwaelimisha jinsi gani wataweza kutambua hayo maradhi.

"Hadi sasa tunapozungumza, watu wengi wanajitambua wanaweza kuepuka na mgonjwa anakuja akiwa hatua za mwanzo kabisa [1 na 2], ambazo inaweza kutibika.

Amesema kwa sababu hiyo MEWATA iliona vema kujenga hospitali kwa nia njema ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kusogeza huduma kwa wananchi zaidi ili kuimarisha afya ya jamii.

"Tunatarajia kujenga hospitali [WWC] katika eneo hili ambalo lilipatikana kwa msaada wa Serikali ya Japan kupitia kwa Mke wa Rais Mstaafu [Jakaya Kikwete], Mama Salma Kikwete," amesema.

Ameongeza "Kwa kweli tunamshukuru sana na tulisema leo katika haya matembezi ni ya kwanza MEWATA kufanyika, tukasema hatuwezi kuja bila kumleta Mama Salma aje kushuhudia siku ya leo.

"Tunatambua Serikali yetu sikivu inafanya mengi, maboresho mengi katika huduma ya afya.

"Hivyo tunapenda kumpongeza na kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mapambano haya ya afya ya mama na mtoto," amesema.

Dkt. Zaitun amesisitiza "Tunakupongeza Waziri Ummy kwa dhamana uliyopewa na tunaona unaiweza 'we are so proudy of you'.

Amesema MEWATA ina wanachama wengi waliotawanyika nchi nzima na inatamani kufikia wananchi wengi zaidi na tunaamini uwezo huo tunao.

"MEWATA tuna moyo wa kujitolea, sisi tupo ... tunaomba ushirikiano ikiwemo kushirikishwa kwenye kutoa huduma za afya, pili 'support' ya ki-fedha kuweza kufikisha huduma hizi.

"Maana tunasema huduma bure lakini ili kufanikisha kuna watu wengine wanakuwa wanazigharamia, kwa hiyo tunaomba mtushike mkono, mtupe 'support' kubwa," ametoa ombi.

Ameongeza "Tunaomba utusaidie kufanikisha kujenga Well Women Center [WWC] ambayo kwa maneno yako unasema iwe 'wellness center'.

"Hii itakuwa imejumuisha mambo mengi, si tu saratani, rehabilitation, counseling na mambo yote yatakuwepo," amesema na kubainisha hospitali hiyo itatoa huduma kwa jinsi zote.

Akizungumza Mama Salma amewapongeza MEWATA kwa kuendelea kuitumikia jamii kwa kuifikishia elimu sahihi na uchunguzi wa awali wa magonjwa hayo.

Ameipongeza pia Serikali kwa kufanya kazi kubwa na nzuri ya kuimarisha mfumo wa huduma za afya nchini kuanzia ngazi ya Taifa hadi msingi.

"MEWATA mmefanya kazi nzuri kufikia malengo ambayo mlijiwekea katika mapambano dhidi ya saratani ya kizazi na matiti na kuhamasisha vijana kusoma udaktari," amesema.

Ameihimiza jamii kuendelea kujitokeza kufanya uchunguzi wa awali kwani wakigundulika mapema watatibiwa na hatimaye kupona.

".., kwa kuwa mgeni rasmi ni Ummy ana uwezo mkubwa wa kuongea na watu duniani na mkajenga msingi.

"Uwezo huo anao hata akienda kwa mama anamwambia unajua kule kuna kiwanja sasa tunafanyaje, ana mtandao mpana hili halimshindi," amesema.

"[MEWATA] tulianzisha na moto na nataka moto ule ule tuuendeleze," amesisitiza Mama Salma ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Mtama.

Waziri Ummy amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imepokea wazo hilo lenye tija kwa jamii la ujenzi wa hospitali ya WWC.

Amesema hivi sasa Tanzania inakabiliwa na janga la ongezeko la visa vya magonjwa yasiyoambukiza [NCD's] ambayo yanaathiri idadi kubwa ya watu na hata vifo.

"Saratani ya mlango wa kizazi katika kila watu 100 kuna  watu 25 wanaugua, saratani ya matiti kuna watu 10 wanaugua katika kila watu 100," amesema.

Amesisitiza bado kuna wengi wanakabiliwa na magonjwa ya Kisukari, Shinikizo la Damu pamoja na mengineyo yaliyopo kundi hilo la NCD's.

"[Hivyo] leteni andiko lenu, andiko zuri ili wadau waweze kuchangia fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kituo hiki," amesema.

Ameipongeza MEWATA kwa kazi kubwa na nzuri inayofanya ambayo waliianza takrbani miaka 20 iliyopita katika kuifikia jamii na kuihudumia.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement