moja

Responsive Advertisement


Na Veronica Mrema

Afya ya jamii ngazi ya msingi inakwenda kuimarishwa kwa kasi zaidi nchini, ni eneo lililotazamwa kwa 'jicho' la tatu na Shirika la Afya Duniani [WHO - Tanzania].

Nguzo kuu nne zimewaleta pamoja, mezani WHO - Tanzania na taasisi 11 zisizo za kiserikali [NGO's] na kuweka saini ya makubaliano maalum [MoU] ya utendaji kazi wa pamoja.

Ushirikiano huo wa dhati umesainiwa leo Ofisi Kuu za Umoja wa Mataifa [UN - Tanzania] zilizopo Dar es Salaam kati ya WHO - Tanzania na taasisi hizo.

Lengo kuu la MoU hiyo ni kuimarisha huduma za afya ngazi ya msingi ili kufikia agenda ya lengo namba tatu la Maendeleo Endelevu ya Dunia [UN-SDG's] linalohimiza Afya kwa Wote [UHC].

"Tunaangazia pamoja uimarishaji wa mifumo ya afya ili kuwepo usawa katika utoaji huduma na kwa ubora," Mwakilishi Mkaazi wa WHO - Tanzania Dkt. Charles Sagoe ametaja na kusisitiza,

"Tutashirikiana na taasisi hizi zisizo za kiserikali katika kuboresha huduma, kuimarisha nguvu kazi na matumizi ya teknolojia kwenye utoaji huduma za afya," amesema.

Ametaja eneo jingine ni udhibiti wa magonjwa hususan ya milipuko ambayo kwa sasa yamekuwa tishio pamoja na magonjwa yasiyoambukiza.

"Tutafanya pamoja kuzuia na kudhibiti magonjwa, kuhimiza afua ya chanjo na kuchagiza mtindo bora wa maisha kwa jamii ya Watanzania,".

Dkt, Sagoe ametaja eneo jingine ni la afua za kinga kwa ujumla wake kwamba watajikita kwa pamoja kuifikia jamii kubwa ya Watanzania.

"Kwa kuwapa elimu ya afya kwa ujumla wake, kuzingatia lishe bora, usafi wa mazingira na masuala ya afya ya uzazi,". amebainisha.

Amesisitiza kwa kuingia makubaliano hayo ni rasmi sasa kwamba WHO - Tanzania na taasisi hizo wanakwenda kuimarisha afya katika ngazi ya jamii.

"Kwa sababu eneo la ubunifu pia tutalipa kipaumbele katika utekelezaji wa MoU hii pamoja na tafiti ili kuleta masuluhisho kwa changamoto mbalimbali za afya zinazoikabili jamii," amesema.

Makubaliano ambayo WHO - Tanzania imeingia leo na taasisi hizo 11 zisizo za Kiserikali utekelezaji wake ni kuanzia mwaka huu 2024 na 2025.

Dkt. Sogoe amesisitiza "Utaisaidia Tanzania kufanya mageuzi makubwa kwa raia wake kufikia lengo la dunia [SDG's namba 3] kuhakikisha inapata Bima ya Afya kwa Wote -Universal Health Coverage].

Akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika hafla hiyo, Dkt. Ambele Mwakilango kutoka Maabara Kuu ya Taifa, amesema MoU ina manufaa makubwa kwa Tanzania.

Amesema itakwenda kusaidia kutatua changamoto kadhaa zinazoikabili sekta ya afya kwani inaenda sambamba na vipaumbele vyake vya hivi sasa.

"Wizara ya Afya ni sehemu ya kuunganisha wadau na kufanya kazi kwa pamoja, tunaangalia iwapo kazi wanazotekeleza zinakidhi vigezo," amesema.

Amebainisha Wizara ina wajibu wa kuangalia pia uwiano sawia katika utendaji kazi katika utoaji wa huduma kwa jamii.

"Changamoto ilikuwa kila mdau ana tekeleza kazi zake kwa peke yake, hii inawaleta pamoja hivyo tunaweza kujua wapi kuna uhitaji mkubwa na tupunguze ili kuweka usawa," amesema.

Ameongeza "Hivyo, WHO Tanzania wametusaidia mno kwa tukio hili la leo na tutafanya kazi kwa pamoja kwa ufanisi zaidi.

"Tunatarajia wataenda kufanya kazi ya kuhimiza elimu ya Bima ya Afya kwa Wote na watatusaidia pia kujua wapi tuweke uwiano mzuri katika rasilimali watu kwenye sekta ya afya,".

Taasisi zilizosaini MoU na WHO Tanzania hii leo ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam [Ndaki ya Elimu - DUCE], Catholic Relief Services [CRS] na Doctors with Africa [CUAMM].

Nyingine ni SIKIKA, Chuo Kikuu Mzumbe, AMREF Health Afrika - Tanzania, Ifakara Health Institute, na International Rescue Commitee.

Taasisi nyingine ni Raising Up Friendship Foundation [RUFFO] na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili [MUHAS].

Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali [NaCoNgo] Racheal Chagonja amesema MoU hiyo ina tija kwa Tanzania.

"Tunashukuru na tunafurahi sana, kushuhudia utoaji saini huu baina ya WHO Tanzania na NGO's za hapa Tanzania.

".., kwetu sisi ni tija kubwa kwa sababu inaleta chachu katika jitihada za NGO's yameendelea kufanya katika kuhamasisha na kuchagiza maendeleo katika sekta ya afya Tanzania.

"Kwa sababu itaongeza rasilimali kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa NGO's katika Tanzania.

Amesisitiza "Hasa katika maeneo ambayo Serikali inakuwa inapata changamoto kuyafikia kirahisi, kwa sababu NGO's nyingi zipo kwenye jamii.

"Hivyo, tunaamini utoaji saini MoU ya leo itakuwa kuchagiza zile kazi ambazo jitihada zinafanywa na Serikali katika vipaumbele vyake, katika 'system'.

"Elimu ya afya na kuongeza chachu ya ushawishi wa mijadala na mabadiliko ya kiserikali katika [ufanisi zaidi wa] utendaji kazi wa sekta ya afya.

📸 WHO - Tanzania

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement