moja

Responsive Advertisement


Dodoma

Silaha mbili za moto zilizokuwa zikitumiwa kulinda mashamba ya bangi, zimekamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya [DCEA - Kanda ya Kati] na kukabidhiwa kwa Jeshi la Polisi Dodoma.

DCEA ilikamata silaha hizo mbili kwenye operesheni zilizofanyika tarehe 24 hadi 28 Aprili,2024 mkoani humo. 

Mbele ya waandishi wa habari, leo katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi [RPC] Mkoa wa Dodoma, Kaimu Kamishna Msaidizi Kanda ya kati Mzee Kasuwi amesema, 

".., silaha hizo aina ya gobore zilikuwa zinamilikiwa na Hamisi Chambo (46) na Abdilah Juma (45) wote wakazi wa kata ya Segera.

Ameongeza "Silaha zilikuwa zikitumika kulinda mashamba ya bangi. Maeneo ya Wilaya ya Chamwino na Dodoma Mjini.

Pamoja na silaha hizo haramu, jumla ya ekari 9.5 za mashamba ya bangi nazo tayari zimeteketezwa.

DCEA pia ilikamata kilogramu 156.23 za bangi na misokoto 127 ya bangi ambapo watuhumiwa 16 wanashikiliwa kuhusika na dawa hizo.

Kamishna Kasuwi amewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu ambao wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya kwa kupiga simu bure kupitia namba 119.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa  Dodoma [RPC] Theopista Mallya ameishukuru DCEA kwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kutokomeza uhalifu.

Ametoa rai kwa wananchi  kufuata Sheria za Nchi na taratibu zake kwani Jeshi la polisi lipo na litaendelea kutokomeza matumizi ya dawa za kulevya.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement