moja

Responsive Advertisement
Dar es Salaam 

Ni kwa mara ya kwanza Tanzania imetoa mgombea wa nafasi ya kiti cha Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika [WHO-Afro].

Sekta ya afya inazidi kupiga hatua katika duru za Kimataifa ambapo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemchagua Dkt. Faustine Ndugulile kuwania kiti hicho.

Historia kubwa ya kipekee na adhimu kwa sekta ya afya itaandikwa, endapo ataibuka kidedea Daktari huyo mwenye uzoefu na ujuzi mkubwa katika masuala ya afya duniani.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu mapema leo ameongoza uzinduzi wa kampeni maalum kwa nafasi hiyo aliyopendekezwa Ndugulile ambaye ni  Daktari wa Taaluma hiyo.

"Mkurugenzi wa WHO-Afro anayemaliza muda wake wa miaka 10 anatokea nchini Botswana ukanda wa SADC," amesema na kuongeza

"Kwa Tanzania ni mara ya kwanza tunagombea nafasi hiyo na tunaamini kabisa tutashinda nafasi hiyo kutokana na aina ya mgombea ambaye tumemuweka,".
Waziri Ummy amesisitiza “Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinafanya vizuri sana duniani katika mapambano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukiza.

"Pamoja na kuimarisha huduma za afya ya uzazi mama na mtoto, Tanzania tumefanikiwa kupunguza vifo vya wanawake wajawazito kwa zaidi ya 80%,".
Amesema Tanzania ina mfumo mzuri sana wa kuimarisha huduma za Afya ngazi ya msingi kuanzia Zahanati, Vituo vya Afya pamoja na Hospitali za Halmashauri.

"Hivyo itakwenda kubadilishana uzoefu huo na nchi nyingine za Afrika,".
Naye, Dkt. Ndugulile amemshukuru Mhe. Rais Samia kwa kupendekeza jina lake na kuridhia kugombea katika nafasi hiyo. 

“Nafasi hii inasimamia nchi 47 katika Bara la Afrika, Tanzania tunafanya vizuri sana katika Sekta ya Afya na tuna mafanikio makubwa ya kuigwa.
"Tunataka na sisi tuende tukayaeneze yale mazuri yetu kwa wengine ili kuweza kusimama pamoja," amesema.

Ameongeza "Vipaumbele vya nchi ambavyo ni pamoja na kuendelea kuboresha huduma za Afya katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.

".., ni eneo ambalo Tanzania tumefanya vizuri, nchi nyingi za Afrika bado wana changamoto hiyo. 
Amesema Tanzania inataka ikasimamie kujenga mifumo imara ambayo itaweza kuhimili athari za magonjwa ya milipuko.

"Pamoja na majanga mengine ambapo kwa Bara la Afrika limeathirika sana na magonjwa hayo," amebainisha.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Januari Makamba akizungumza jambo wakati wa hafla hiyo, amesema hii leo wamepokea barua rasmi, nchi zote za SADC zinaunga mkono.

"Zimemuunga mkono Dkt. Ndugulile na tayari imeanza kampeni na kuna nchi kama saba ambazo zimeahidi kumuunga mkono.

Amesisitiza "Hivyo tayari tuna kura 27 [yaani] tayari tuna nusu ya kura katika mchakato huo.

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement