Recent Post


 


moja

Responsive Advertisement


SUDV ni kifupi cha maneno 'Sudan Ebola Virus', yaani kirusi cha Ebola aina ya Sudan, Ukanda wa Afrika Mashariki umekuwa katika mapambano dhidi ya maambukizi ya aina hii ya kirusi cha Ebola.

Mlipuko wa kirusi hicho uliripotiwa kuzuka huko Uganda tangu Septemba 20, mwaka huu katika Kijiji cha Madudu kilichopo ndani ya Wilaya ya Mubende nchini humo.

Ndani ya kijiji hicho kiliripotiwa kisa cha kwanza cha mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 24 na visa vingine vikazuka na kuripotiwa katika maeneo mengineyo likiwamo Jiji la Kampala.

Tangu hiyo Septemba 20, mwaka huu hadi kufikia sasa Uganda imeripoti visa vya watu wapatao 142 waliambukizwa virusi hivyo, kati yao watu 56 wamefariki dunia.

 

Uganda imekuwa ikipambana kuzuia na kudhibiti kusiendelee kuzuka visa vipya na hata kuzuia maambukizi hayo yasivuke mipaka kwenda katika mataifa mengine jirani ikiwamo Tanzania.


"Tathmini ya Shirika la Afya Duniani, Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyopo katika Ukanda huu ambayo tupo katika kundi la hatari zaidi kuweza kupata maambukizi ya Ebola," alinukuliwa na vyombo vya habari Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu.

 

Kwa mujibu wa Waziri Ummy, hali hiyo ni kwa sababu ya muingiliano mkubwa wa idadi ya watu na ndiyo maana imechukua hatua nyingi madhubuti kuhakikisha ugonjwa huo hauingii nchini.

 

Ebola ni miongoni mwa magonjwa tishio ya mlipuko duniani linaeleza Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Afya, likibainisha kuna aina tano za virusi vya Ebola.

Aina hizo ni bundibugyo ebolavirus (BDBV), zaire ebolavirus (EBOV), reston ebolavirus (RESTV), sudan ebolavirus (SUDV) na tai forest ebolavirus (TAFV).

Kulingana na wanasayansi, aina tatu za virusi {BDBV, EBOV na RESTV}, ndizo ambazo huongoza  kusababisha mlipuko wa ugonjwa huo barani Afrika.

Kirusi kilichozuka Uganda wanasayansi wanasema ni ‘Sudanese’, hiki kinatajwa kuwa hatari zaidi na kilipozuka dunia haikuwa na chanjo yoyote ya kukidhibiti.

Taarifa nyingine inayohusiana Ebola isiyo na chanjo tishio, muingiliano wa watu waiweka ‘pabaya’ Tanzania (matukionamaisha.blogspot.com)

Ingawa ripoti za Wizara ya Afya nchini humo zinaonesha hali imetulia kwa wastani kwani kwa zaidi ya siku 45 sasa hakuna kisa kipya kilichoripotiwa.

Wanasayansi wanakitazama kirusi aina ya ‘SUDV’ ni cha tishio zaidi kwa sasa kwani bado hakuna chanjo iliyothibitika kuweza kukabili kirusi hicho.

Wanasayansi waligundua kirusi cha Ebola mnamo mwaka 1976 katikati ya msitu wa kitropiki wa Jamhuri ya zamani ya Zaire ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanasayansi waligundua pia aina ya kirusi ambacho kimesababisha asilimia takriban 80 ya milipuko yote ya ugonjwa huo.

Kulingana na wanasayansi ilibainika pia katika janga baya la mlipuko wa ebola lililotokea Afrika Magharibi kati ya 2014 na 2016 na lililosababisha vifo 10,000 lilitokana na aina hii ya kirusi cha ebola.

Kutokana na janga hilo aina mbili za chanjo na aina mbili za dawa dhidi ya kirusi hicho cha Zaire zilivumbuliwa.

Ni katika mwaka huo huo {1976} ambapo pia wanasayansi waligundua aina nyingine ya kirusi cha Ebola ambacho ni SUVD wakati walipokuwa wakifanya tafiti zao. 

Aina hii ya kirusi cha Sudan ni nadra sana, hata kilivyoripotiwa sasa huko Uganda ni baada ya kupita kwa miaka mingi tangu kilipogundulika.

Shirika la Afrika duniani WHO lilitambua kitisho kwamba mlipuko wa ebola unageuka kuwa tatizo kubwa kwa taifa hilo la Afrika Mashariki na unaongezeka. 

Ndiyo maana, kuwasili kwa shehena ya dozi 1,200 za chanjo nchini humo dhidi ya kirusi hicho kunaandika historia mpya na matumaini kwa wanasayansi kutokomeza kabisa maambukizi ya kirusi hicho.

Desemba 8, mwaka huu, Waziri wa Afya wa Uganda Jane Ruth Aceng aliongoza mapokezi ya shehena hiyo kutoka kwa WHO.

Tunafuraha sana kwamba Uganda leo imepokea dozi 1,200 za chanjo moja kati ya tatu ambazo zitatumika dhidi ya aina hii ya virusi vya Ebola,” amenukuliwa Waziri huyo na vyombo vya habari.

Chanjo hiyo na nyinginezo mbili zimeridhiwa na WHO na ipo katika hatua ya majaribio ya kitabibu, zimetengenezwa na Taasisi ya Sabin iliyoko Marekani kwa msaada wa mamlaka ya Marekani.

Chuo Kikuu cha Oxyford na Taasisi ya Jenner ya nchini Uingereza pamoja na Taasisi ya Serum ya India nazo zimetengeneza aina nyingine pamoja na Shirika la utafiti wa kisayansi la International AIDS Vaccine Initiative (IAVI).

“Mgonjwa wa mwisho aliruhusiwa kutoka hospitalini Novemba 30, mwaka huu nchini humo.

“Kwa hatua hii ni kwamba sasa imeanza kuhesabu siku, kuelekea mwisho wa janga hili,” anasema Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika Matshidiso Moeti.

WHO imeeleza chanjo hiyo itatolewa kwa watu walio katika hatari zaidi ya kuambukizwa ugonjwa huo kupitia mradi ujulikanao kama ‘Tokomeza Ebola’, watapatiwa kwa hiyari.

Hata hivyo, bado hakuna chanjo zilizoidhinishwa za aina ya Ebola ya Sudan ambayo inasababisha maambukizo hatari nchini Uganda.

Majaribio hayo yatabainisha kama mojawapo au zote tatu zinafaa katika kupambana na ugonjwa huu. 

Post a Comment

saba

nane


 


sita

Responsive Advertisement